MANJU DUOX YAJIGAMBA KWA UBORA WA BIDHAA BORA MAONESHO YA SABASABA


Bidhaa zinazopatika katika banda la Taasisi ya "The warrior Women katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba.
Mkurugenzi wa Taasisi ya The warrior Women Sabra Machano akitambulisha Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo kwa  Mfanyabiashara wa juisi ya Matunda mbalimbali katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam

Na Khadija Seif Michuzi Tv 

TAASISI  ya The warrior Women yawakaribisha wajasiriamali na wapenzi wa bidhaa zao  katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam.

Akizungumza na Michuzi Tv Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sabra Machano amesema kupitia Taasisi ya The warrior Women inalenga kuwakwamua wajasiriamali wadogo wadogo kutoka sehemu mbalimbali.

"Katika Maonesho ya Sabasaba tumeanza kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo hasa wa vyakula Kuna juice,viungo vya vyakula,urojo pamoja na bidhaa za urembo kwa ujumla."

Machano amesema kwa Sasa ameanza na wafanyabiashara wachache kadri muda unavozidi kwenda wataweza kuongeza na wafanyabiashara wengine kwa Mikoani hasa Arusha,Dodoma na Mikoa mengine.

Hata hivyo kwa upande wake Mmoja wa wajasiriamali ambao kupitia Taasisi hiyo imewapa nafasi ya kuonyesha bidhaa zao katika Maonyesho hayo Zuwena Ally maarufu kama Manju duox ambae anatengeneza bidhaa za viungo vya chakula pamoja na bidhaa za urembo.

"Ni nafasi pekee ya kutambulisha bidhaa zetu ambazo ni Bei nafuu na bidhaa Bora kuliko zote katika Maonyesho haya na inatupa  fursa ya kuweza kuwafikia wateja wetu kwa haraka na kuuza kwa wakati."

Pia Manju duox ameongeza kuwa fursa kama hiyo ni muhimu kwani mbali na kupata nafasi ya kuuza bidhaa Bali pia inampa fursa mfanyabiashara kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine na kutanua kimasoko zaidi.


No comments: