WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA VIONGOZI VYAMA VYA KIJAMII KUACHA TAMAA, UKOROFI, ASULUHISHA MGOGORO SUGU WA UMOJA WA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI NCHINI, WAFANYA UCHAGUZI, WAIPONGEZA SERIKALI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wanachama wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO) baada ya kusuluhisha mgogoro sugu wa Umoja huo uliosababisha kuvunjika kwa Katiba. Mkutano Mkuu wa Umoja huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya African Dreams, jijini Dodoma, leo. Amewataka viongozi waliochaguliwa waongoze kwa busara na endapo kundi lolote likijitokeza kufanya vurugu Serikali itawashughulikia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wanachama wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO) baada ya kusuluhisha mgogoro sugu wa Umoja huo uliosababisha kuvunjika kwa Katiba. Mkutano Mkuu wa Umoja huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya African Dreams, jijini Dodoma, leo. Amewataka viongozi waliochaguliwa waongoze kwa busara na endapo kundi lolote likijitokeza kufanya vurugu Serikali itawashughulikia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Umoja huo katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya African Dreams, jijini Dodoma, leo, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati) kuzungumza na Wanachama (hawapo pichani) kuhusu mgogoro ulioleta vurugu ndani ya Umoja huo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Youstor Ntungi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda, alipokuwa akimshukuru Waziri huyo kwa kusuluhisha mgogoro sugu wa Umoja huo ambao una zaidi ya miaka sita. Umoja huo tayari umepata viongozi wapya baada ya viongozi wa awali kuondolewa madarakani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda, wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya African Dreams, jijini Dodoma, leo, kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Umoja huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Mwandishi Wetu, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema vyama vingi vya kijamii vinakufa nchini kwasababu ya tamaa pamoja na ukorofi wa baadhi ya viongozi ambao hawana sifa ya kuwa viongozi.

Amesema uongozi ni karama na sio kila mtu anapaswa kuwa kiongozi, hivyo baadhi ya viongozi wanaouongoza jumuiya hizo za kijamii wanashindwa kuwa waadilifu, wanaongozwa na tamaa na kuharibu mipango imara ya umoja wao na kusababisha migogoro kuibuka.

Waziri Simbachawene ameyazungumza hayo, katika ukumbi wa Hoteli ya African Dreams, jijini Dodoma, leo, baada ya kusuluhisha mgogoro sugu wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO) uliodumu kwa muda wa miaka sita.

Mgogoro huo sugu ulisababisha mkutano mkuu kuzuiwa usifanyike kwa nyakati tofauti kutokana na pande mbili za umoja huo kutokukubaliana, ndipo Waziri Simbachawene akaagiza mkutano ufanyika na ajenda kuu ya mkutano huo iwe kufanyika kwa uchaguzi mkuu, na atakuja kuzungumza na wananchama hao baada ya uchaguzi huo kufanyika.

“Leo nimekuja hapa nikiwa na furaha, narudia tena nazungumza nanyi nikiwa na furaha kwasababu sasa mmefanikisha kupata viongozi wenu ambao tunatarajia wataleta maendeleo ya umoja wenu, nyie mnaisaidia Serikjali, kama sera yenu inavyosema hamfanyi biashara bali mnatoa huduma, kwa niaba ya Serikali na Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan nachukua nafasi hii kuwapongeza sana kwa kufanya uchaguzi wa viongozi halali, ya zamani yamefutika, sasa aanzeni upya,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya watu watakao leta fujo, na pia viongozi waliochaguliwa Pamoja na wanachama wote wanapaswa kufuata na endapo kuna mapungufu wayarekebishe na wasonge mbele.

Alisisitiza kuwa, panapotokea amani na utulivu katika familia ndio mafanikio yanapatikana lakini unakuta baba ndio mcheza sarakasi  za fujo kila siku, na hiyo inatokana kwasababu hakuzaliwa kuwa kiongozi.

“Uongozi unaanzia chini kabisa, ukimpa uongozi wa Jumuiya mtu anaelewa madaraka lazima atawasumbua tu, utafika wakati wa uchaguzi hataki uchaguzi ufanyike, na ndio jumuiya nyingi zipo hivyo, atazuia hiki atazua kile,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja huo, Alfred Luvanda alisema kitendo cha waziri Simbachawene kusuluhisha mgogoro huo ameleta furaha ndani ya umoja huo, na wananchama wamekuwa na furaha kubwa.

“Mheshimiwa Waziri ni mtu mwenye busara, hekima, tunakushukuru sana kwa hapa tulipofikia, tumefanya uchaguzi na viongozi wamepatikana, tunasema asante sana kwa Serikali kutufanikishia Umoja wetu kuweza kusonga mbele,” alisema Luvanda.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Youstor Ntungi alisema baada ya mgogoro kumalizwa na Waziri Simbachawene, wanachama wamepata ari na moyo wa kuimarisha Umoja wao ili kuondoa ubadhirifu wa fedha uliokuwa umeshamiri, kukifanya chama kuwa mali ya watu wachache na hivyo kudumaza juhudi za umoja huo kupigania maslahi ya wanachama wake kutokana na migogoro ya uongozi isiyokwisha.

 Ntungi aliwataja viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Juni 9, 2021 katika Mkutano Mkuu uliofanyika ni Mwenyekiti Taifa, Alfred Luvanda, Fredrick Otieno, Makamu Mwenyekiti Taifa, Peter Nayar, Katibu Mkuu Taifa, Yusto Segereti- Naibu, Katibu Mkuu Taifa, Delphina Ngirwa, Mweka Hazina, Juliana Kalinga, Naibu Mweka Hazina Taifa, na wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya Tamongsco upande wa wanawake ni Anna Mnazi, na wanaume ni Haji Mohamed.

Lengo kuu la Umoja huo ni kuunganisha mameneja na wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya Serikali Tanzania ili kuboresha utoaji wa elimu katika sekta binafsi na pia kuwa kiungo kati ya wamiliki wa shule na vyuo hivyo na serikali.

 

No comments: