WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU YA WACHANGIA DAMU DIANI JUMATATU JUNI 14
Na Khadija Khamis –Maelezo
Uchangiaji wa damu kwa jamii unasaidia kuokoa maisha ya watu wengi ambao wanakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo kupata ajali, kuishiwa na damu wakati wa kujifungua, upasuaji pamoja na kupungukiwa na damu kwa watoto na watu wazima.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na watoto Dkt. Juma Salum Mbwana wakati akitoa taarifa juu ya umuhimu wa uchangiaji damu huko katika ukumbi wa Wizara hiyo Mnazimmoja.
Amesema damu bado inahitajika katika benki ya damu ili kuondosha upungufu wa damu katika baadhi ya hospitali na kuweka akiba ya kutosha pale inapohitajika.
Amezitaja sababu kubwa za kuhitajia tiba ya damu ni kuokoa maisha ya mgonjwa pale linatokea tatizo ikiwemo ajali na kupelekea kupoteza damu nyingi hivyo husababisha kusaidia ili kumnusuru .
Ameeleza kuwa uchangiaji wa damu unasaidia kupunguza kasi ya maambukizo ya ukimwi na kuziwezesha hospitali kuwa na akiba ya damu za kutosha wakati wowote linapotokea na sio kusubiri itokee dharura.
Dkt. Juma ameisisitiza jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ii kuokoa maisha ya wengine .
Amefahamisha kuwa umri wa kuanza kuchangia damu ni miaka 18 hadi 65 ambapo mchangiaji hapashwi kuwa na maradhi endelevu kama kisukari, shindikizo la damu, maradhi ya moyo, pumu na kifafa.
Nae Meneja Mpango Taifa wa Damu Salama Dkt. Salama Rashid Abdalla amewataka wananchi wenye sifa za kuchangia kujitokeza kwa wingi kwa kuchangia damu hapo kituoni amani na pale popote ambapo wafanyakazi wa benki ya damu watapowafikia katika jamii.
Ameeleza kuwa pindipo wananchi watachangia damu kwa wingi utasaidia kuondosha uhaba wa damu katika benki ya damu pamoja na kukidhi mahitaji kwa wagonjwa ambayo huhitajika zaidi ya chupa 30 kwa siku katika hospitali ya rufaa mnazimmoja.
Alifahamisha kuwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama umezingatia uchangiaji wa damu wa hiyari umeanzishwa mwaka 2005 chini Wizara ya Afya ambapo ujumbe wa mwaka huu ni “Damu ni uhai changia damu uokoe maisha”.
Mkurugenzi Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt. Juma Salum Mbwana akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia Damu Duniani yatakayofanyika Jumatatu june 14 Makao Makuu ya Benki ya damu Sebleni kwa wazee Mjini Zanzibar.
Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Zanzibara Dkt. Salama Rashid Abdalla akijibu maswali ya wandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia Damu Duniani.
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya iliyotolewa kuhusu siku ya wachangia Damu Duniani itakayofanyika Makao Makuu ya Benki ya damu Sebleni kwa wazee Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.
No comments: