WAGANGA WA JADI WAUNGANA NA KUJENGA MADARASA SIMIYU
WAGANGA wa Jadi wa Wilaya ya Itilima wameungana na kujenga madarasa mawili katika shule ya Sekondari Chinamili.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila amewapongeza Waganga hao wa Jadi kwa mchango wao mkubwa wa maendeleo katika sekta ya elimu kwa kujenga madarasa hayo.
Kafulila amesema ujenzi wa madarasa hayo mawili umeonyesha uthamini wa waganga hao wa jadi katika elimu, na kuondoa dhana ya kwamba waganga wa jadi hawathamini elimu.Hali kadhalika wameunga mkono jitihada za Serikali katika masuala ya elimu.
Vilevile ameeleza kufurahishwa sana na jitihada hizo na kuwataka kutosita kumshirikisha k pindi wanapohitaji msaada na amewaunga mkono kwa kutoa milango miwili ya vyumba vya madarasa hayo.
No comments: