UVCCM MKOA WA MANYARA WAMTOLEA UVIVU MBATIA, MBOWE MADAI YA KATIBA MPYA
Na Mwandishi wetu, Manyara
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Manyara umemtaka Mwenyekiti wa NCCRA-Mageuzi James Mbatia kukumbuka yeye na wenzake wa kambi ya upinzani kukamisha mchakato awa Katiba mpya wakati wa Bunge la Katiba.
Hivyo umemtaka Mbatia kutomuondoa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mstari mnyoofu wa mipango endelevu alionayo wakati huu yenye tija na manufaa umma.Akitoa msimamo huo leo Juni 17,2021, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Manyara Francis Komba amesema kama upinzani imekosa hoja za maana si haramu na wala hawajapata dhambi ikiwa watanyamaza na kuiuunga mkono Serikali ya Rais samia.
Amesema ni jambo gumu upinzani kuikosa Serikali kwa wakati huu ambao imekuwa ikitimiza wajibu wake ipasavyo kwa kuitazama jamii, kuimarisha uhusiano wa kimataifa, ikivutia wawekezaji, ikifungua milango na fursa za kibiashara kitaifa na kimataifa .
"Tunajua jinsi upinzani yanayoendelea kufilisiwa hoja kutoka na ufanisi wa Serikali. Unapokosa kuwa na mitaji wa fedha za kutosha hutafanya biashara zako kwa ufanisi,"amesema.
Ameongeza huwezi hata kupata mkopo kwenye taasisi za fedha, hivyo Kina Mbatia na Freeman Mbowe hawana mitaji ya kisiasa wamebaki wakimangamanga.
Aidha amesema Taifa limefikishwa miaka zaidi ya 50 likiongozwa na Katiba iliyoundwa mwaka 1977 na kama usingekuwa ni Katiba bora yangeweza kutokea mambo mkanganyiko."Unaitiliaje shaka Katiba ambayo imeyalinda maisha ya watu , usalama wao, umoja walionao, maendeleo yao kiuchumi, kisiasa na kijamii .
"Katiba yetu imetoka majibu katika kila swali gumu. Imezingatia matakwa ya utawala, demokrasia, haki, sheria na hata nyakati ngumu za kubadilishana madaraka,"amesema.Amewataka wanasiasa wa upinzani kama wanasoma biashara ya siasa hailipi hawatachekwa na wananchi ikiwa watafungua na kuanzisha biashara nyingine kama za kuuza nyanya, mbogamboga au kuchoma nyama choma ili waachane na siasa.
"Kwanza kujenga chama cha siasa hadi iwe taasisi kamili yenye heshima ni kazi ngumu mno.Tangu mwaka 1992 vyama vya upinzani vimekuwa vikichechemea kwa mwendo wa jongoo na wa kususua. Vimejikwaa, vimedondoka, havitainuka na kusimama,"amesema.
Ameongeza ni jambo la kushangaza kuwasikia tena viongozi wa Chadema na NCCR -Mageuzi wakianza kubwabwaja na kutaka mchakato wa Katiba mpya uanze tena wakati wao ndio wahusika waliowachochea wabunge watoke nje ya bunge maalum la katiba.
"Kazi ya askari ni kupambana vitani. Wanapodondosha chini silaha na kuanza kukimbia hao ni askari waoga na dhaifu. Mbowe, Profesa Ibrahim lumumba na Mbatia walidondosha chini silaha na kulikimbia Bunge maalum la katiba .Kama walimeshindwa kutetea wakiwa ndani ya Bunge huwatetea wakiwa nje ya bunge,"amesema.
UVCCM wameunga mkono msimamo wa CCM uliotolewa na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa wiki iliyopita na kuendelea kuwataka wananchi kuwapuuza wanasiasa hao ambao wameshindwa kuiongoza vyama vyao badala yake wanataka kuiyumbisha nchi.
No comments: