UMOJA WA WATENGENEZA MAGARI DUNIANI WATEMBELEA KIWANDA CHA GFA WILAYANI KIBAHA,WAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO

 Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV


KIWANDA cha Magari cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimepata ugeni mkubwa baada ya kutembelewa na wanachama wa Umoja wa Watengenezaji Magari Duniani(AAAM).

Wakiwa kwenye kiwanda hicho wanachama wa umoja huo wamepata fursa ya kuzungunza na kubadilishana mawazo na viongozi wa kiwanda cha GFA ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia pia kuimarisha uhusiano.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema kwamba Kiongozi wa Msafara wa AAAM ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Nissan ukanda wa Afrika Mike Whitfield  amesema watashirikiana na kiwanda hicho cha GFA katika nyanga mbali mbali na kuweza kujitegemea na suala la uunganishwaji wa magari na Tanzania inakuwa  kama nchi zingine zinazotengeneza magari kama ilivyokuwa nchi ya Afrika Kusini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa  wa kampuni ya GFA Assemblers ,Mehbooub Karmali ameushukuru ujio huo wa msafara wa viongozi hao na kusisitiza ujio wao ni neema kwao na mambo yakienda  vizuri basi Serikali itakuwa inapata fedha za kigeni kutokana na magari kutengenezwa nchini hali itakayoongeza soko la ajira kwa vijana wengi wanao hitimu katika vyuo vyetu.

Wakati huo huo wanachama hao wakiwa nchini Tanzania wamekutana  na viongozi wa Serikali na kuzungumza mambo kadha katika kuhakikisha lengo la Tanzania ya Viwanda linatimia kwa vitendo

Miongoni mwa wanachama wa umoja huo ambao wametembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo na Serikali wanatoka katika kampuni za Nisani,Ford, BMW, Isusu, Toyota na Volkswagen.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GFA Assemblers, Mehbooub Karmali (kulia) akimtembeza moja ya wageni katika kiwanda hicho Kibaha mkoni Pwani
-Mshauri mkuu wa Waziri wa viwanda nchini Afrika ya kusini, Alec Erwin  akizungumza jambo wakati wa ujumbe wa Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia(Association of African Automobile Segment (AAAM) walipotembelea kiwanda cha kuunganisha magari nchini kilichopo Kibaha mkoni Pwani .Kati kati ni Mwenyekiti wa bodi ya GFA Assemblers, Mehbooub Karmal  na kulia ni Mwenyekiti wa umoja wa watoa huduma za mafuta na gesi nchini (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim.
Jopo la viongozi wa  Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia(Association of African Automobile Segment (AAAM) wakiangalia moja ya gari inavyotengenezwa katika kiwanda hicho

No comments: