TASAC YAKUTANA NA WADAU KUJADILI SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Wakala wa Meli nchini (TASAC) limesema kuwa litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi kwa kutoa huduma kwa usafirishaji wa shehena ndani ya nchi na nje ya nchi.
Akizungumza na katika mkutano wa wadau wa usafirishaji nje nchi na ndani ya nchi Mkurugenzi Udhibibiti Huduma za Usafiri wa TASAC Deogratius Mkasa amesema kuna umhimu wa kuwajengea uwezo wa wasafirishaji wa shehena katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kuzitatua.
Amesema kuwa elimu hiyo ni endelelevu wa wadau kwani baada ya kufanya jijini Dar es Salaam watakwenda katika mikoa ya Tanga na Arusha kwa kuweza kurahisisha mawakala wa usafirishaji wa shehena zza kwenda nje pamoja na za nje kuingia nchini.
Mkasa amesema wadau wakisikilizwa lazima kuwe na uwianio wakati Tasac itapotoa uandaji wa kanuni katika sekta hiyo
Mkurugenzi wa Mkuu shirika la wasafirishaji wa Shehena ISCOST Daniel Kiangi amesema kuwa shirika hilo lina wanachama wa Nne ambao ni Tanzania ,Kenya ,Uganda na Zambia ambapo wamekuwa ana ushirikiano na vyombo vya udhibiti ikiwemo TASAC, Bandari pamoja na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wasafirishaji wa Shehena kwa njia ya Maji Ashraf Ghan amesema kuwa usafirishaji wa mizigio kwa njia ya maji unahitaji kuwa na elimu na sio kufanyika kwa holela.
Amesema kuwa kukaa pamoja na Tasac kunaleta afya katika kutatua changamoto ikiwa ni kupunguza kwa gharama kutokana na kujua taratibu zilizowekwa kwa ndani na nje ya nchi pamoja na kufanya kazi kwa weledi kwa pende zote mbili za mdau na mdhibiti.
No comments: