SIKONGE WAAGIZA KUKUSANYA DENI LA TSHS MILIONI 200.6 KUTOKA KWENYE VIKUNDI


Mkaguzi Mkuu wa Nje Mdhibiti Mkoa wa Tabora Hamu Mwakasola akitoa taarifa ya ukaguzi uliofanyia katika Hamlashauri ya Wilaya ya Sikonge katika mwaka 2019/20.



Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wakiwa jana katika kikao cha kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peres Magiri akitoa maelekezo kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuhakikisha wanajibu hoja za kikaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)

Picha na Tiganya Vincent

……………………………………………………………………………………………………………..

NA TIGANYA VINCENT

MENEJIMENTI ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuhakikisha inafutilia na kurejesha kiasi cha shilingi milioni 200.6 ambazo zilikopeshwa kwa kwenye vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.

Agizo hilo limetolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peres Magiri wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) za mwaka wa fedha 2019/2020.

Alisema lazima wakopaji warejeshe fedha hizo ili ziweze kama kutumika kuvikopesha vikundi vingi zaidi.

Aidha Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kwa Watumishi wa Halmashauri waliosababisha hoja kwa sababu ya kutowajibika ipasavyo, uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao, manunuzi yasiofuata taratibu na usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo hasa katika ngazi za chini.

Alitaja baadhi ya hoja zilizoleta dosari ni pamoja na mapato ya ndani yaliyokusanywa kiasi milioni 99 lakini hakikupelekwa benki, hasara ya kiasi cha milioni 11.8 iliyotokana na Halmashauri kwa sababu ya makosa ujazaji fomu na hivyo Bima ya Afya (NHIF) kukataa kulipa.

Magiri alisema eneo jingine ni kuchelewa kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 661.9 ambayo haijakamilika kwa wakati kutokana na kutokuwepo kwa mikakati, hali hiyo imepelekea kupotezwa kwa fedha zilizowekezwa katika miradi hiyo.

Katika hatua nyingine aliwaagiza Menejimenti na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuongeza nguvu ya ukusanyaji mapato kwa kuwa hadi kufikia tarehe 11 Juni, 2021 kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kilikusanywa sawa na asilimia 70 kati ya makisio yaiasi cha shilingi bilioni 2.7

Alisema Halmashauri ilipaswa kuwa imekwisha kukusanya kuanzia asilimia 90 na kuongeza kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2021 wawe wamekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100.

Magiri alisema dhamira ya Serikali ni kuwa Halmashauri zote zinapwa kujiendesha zenyewe bila ruzuku toka Serikali Kuu kuanzia mwaka 2025, kwa mapato yanayokusanywa katika Halmashauri yako ni dhairi itashidwa kujiendesha.

Magiri alisema nguvu ya zaida inahitajika katika ukusanyaji wa mapato, kubuni vyanzo vipya vya mapato, kusimamia na kuzuia uvujaji wa mapato na kulifanya zoezi la ukusanyaji wa mapato ni la wote kuanzia Wahe. Madiwani hadi kwa Watendaji wa Halmashauri, Kata na Vijiji.

No comments: