Na Humphrey Shao, Michuzi TV

 Imeelezwa kuwa matukio mengi ya uhalifu kwa sasa yamekuwa yakifanywa na watoto wenye umri chini ya miaka 20 jambo ambalo linaashiria kuwa wazazi na walezi kushindwa kutekeleza majukumu yao Ipasavyo .

 Hayo yameelezwa  leo Mkoani Dar es salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chanika Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Joseph Mwakabonga wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanywa na Taasisi inayojihusisha na malezi ya watoto walio hatarini kupoteza malezi ya wazazi SOS, ambapo amesema ni muhimu kwa wazazi kutekeleza wajibu wao.

 “Jeshi la Polisi limekuwa likikabiliana na uhalifu unaofanywa na watoto kwenye mitaa mbalimbali hivyo amewataka jamii kushirikiana na Taasisi za malezi katika kulea watoto kwenye maadili kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo elimu na makazi salama”. Amesema Mwakabonga.

 Kwa upande wake Kaimu meneja mradi kutoka SOS Celestino Mwalongo amesema maadhimisho haya yatumike kuwakumbusha wazazi na walezi kutekeleza majukumu yao.

 Amesema kuwa Tasisi ya SOS imeweza kusaidia jamii ya kuweza kuwalea Watoto katika malezi salama hili waweze kuwa sehemu ya jamii bora .

 Naye Mshololo Ondit kutoka Taasisi ya mazingira forum cc aliposhiriki maadhimisho hayo amezungumzia u.uhimu wa utunzaji mazingira ili watoto waolewe kwenye mazingira safi na salama.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chanika Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Joseph Mwakabonga akizungumza na Wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanywa na Taasisi inayojihusisha na malezi ya watoto waliohatarini kupoteza malezi ya wazazi SOSKatika Viwanja vya Chanika Mnadani.

Kaimu meneja mradi kutoka SOS Celestino Mwalongo akieleza namna Tasisi yake inavyoshiriki katika ukombozi wa malezi ya mtoto wakati wa Mahadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.

Sehemu ya Washiriki waliofika kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya mnadani Chanika.

No comments: