MIMBA ZA UTOTONI, UBAKAJI VIKWAZO VINAVYOWAKABILI WATOTO WA KIKE WILAYANI MKINGA MKOANI TANGA
KAIMU Mkuu wa wilaya ya Mkinga Erick Farahani ambaye ni Afisa Tawala wa wilaya ya Mkinga akizungumza wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa lililofanyika wilayani humo na kuandaliwa na Shirika la World Vision kwa kushirikiana na Halmashauri wilaya hiyo
Mwakilishi wa Wordvision Tanzania ,Agatha Matumaini akizungumza wakati wa Kongamano hilo
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ajari Mwarimwengu akizungumza wakati wa kongamano hilo
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga akizungumza wakati wa Kongamano hilo
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Mkinga Sosten Mtena akizungumza wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa 2021 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo.
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiandamana wakati kongamano hilo
MIMBA za Utotoni, Ubakaji, Ulawiti na ukosefu wa elimu ya jinsi ya afya na uzazi ni miongoni mwa vikwazo vinavyowakabili watoto wa kike wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Hayo yalisemwa na Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Mkinga Sosten Mtena wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa 2021 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo.
Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Mkinga lililowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi, walimu na wazazi.
Alisema kwamba vikwazo vingine ni usafirishaji haramu wa watoto kwenda nchi jirani ya Kenya kutoka Bukoba ikiwemo kuchomwa kwa watoto vitendo ambavyo vinapelekea kukosa haki zao za msingi.
“Kwa mfano Mimba za Utotoni (katika mwezi Machi 2020 hadi may 2021) Jumla ya kesi 37 za Mimba ziliripotiwa jambo ambalo linakwamisha watoto kushindwa kutimiza ndoto zao hivyo niiombe jamii ibadilike”Alisema
Afisa Ustawi huyo alisema ili kuweza kumaliza vitendo vya namna hiyo lazima jamii ibadilike na kuachana tabia hiyo ikiwemo kuvikemea visiweze kujitokea wakati mwengine.
Hata hivyo alieleza watoto waliopo katika mazingira hatarishi kwa kunyimwa haki zao ni wanaoishi na wazee sana,wanaishi na walezi,wazazi ambao hawajiwezi,walio kwenye mapigano au vita,ambao ni wakuu wa kaya,watoto wa kike,wamitaani ,yatima na wale ambao wanafanya kazi viwandani au migodini.
“Lakini zipo athari zinazowakabili watoto ikiwemo unyanyasaji na uzalilishaji, watoto kutumikishwa kingono, kutekelezwa, kunyimwa kwenda shule au kupekekwa shule na mila na desturi potofu zenye madhara kwa watoto”Alisema
Awali akizungumza wakati wa kongamano hilo,Mwakilishi wa Wordvision Tanzania ,Agatha Matumaini aliwaomba viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto na inapotokea mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili watoe taarifa bila kujali lolote.
“Kwani inakuwa ni vibaya na inauma watoto anafanyiwa ukatili na mzazi anashirikiana na mhalifu kuweza kumaliza hilo suala jambo kimya kimya huo ni ukatili kama ilivyo mwengine”Alisema
Alisema Shirika hilo kwa kushirikiana na wadau ikiwemo serikali na halmashauri kwenye kamati za ulinzi wa mtoto wameweza kusaidia kwenye mambo ya afya na lishe.
Hata hivyo alisema watoto 75 walikutwa wana shida lakini kwa ushirikiano wa afya na shirika hilo watoto waliweza kuwekewa mfumo maalumu wa kulishwa na baadae kurudi kwenye hali zao za kawaida na wanaendelea vizuri.
Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mkinga Erick Farahani aliwataka wazazi na walezi kuungana kwa pamoja kukataa na kumekea vikali vitendo vya ukatili kwa watoto ambavyo vinawakwamisha kufikia ndoto zake
"Pamoja na kukemea kwa muda mrefu vitendo vya kikatili ,viovu kwa watoto lakini bado vinaendelea hivyo wataendelea kuvikemea na kuvikataa kwa nguvu zote kwa lengo la kuhakikisha vinatoweka kwenye jamii "Alisema
Hata hivyo alisema pia wanapigana na vitendo vya watoto wadogo kuuza bidhaa ndogo ndogo ikiwemo maandazi,ndizi na katika muda ambao walitakiwa kuwa shulenijambo ambalo linawanyima haki yao ya msingi kupata elimu bora.
"Lakini suala la Ubakaji,Mimba za utotoni bado tunavikataa na katika hili nawaomba wazazi na walezi tuungane kwa pamoja kukataa na kumeea maana kumeibuka tabia kunapotokea mtoto amepewa mimba wanamalizina kifamilia badala ya kuacha sheria ichukue mkondo wake hivyo lazima tulikatae na kulipinga"Alisema
No comments: