KAMPUNI YA JATU PLC YAENDELEA KUCHANJA MBUGA MKOANI DAR, WANANCHI WAENDELEA KUNUNUA HISA
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KAMPUNI ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini(JATU PLC)wameendelea na kampeni yao ya kuhamasisha wananchi wa Dar es Salaam kununua hisa za kampuni hiyo ambazo zinalenga kuwaokomboa kiuchumi.
Hivyo leo Juni 16, JATU wamekutana na wafanyabiashara na wananchi waliopo Stendi ya Mabasi ya Mikoani maarufu kwa jina la Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Mwisho pamoja na wananchi wa Mabibo mkoani Dar es Salaam .
Wakiwa maeneo hayo wafanyabiashara na wananchi wameonekana kuchangamkia kununua hisa za JATU PLC baada ya maofisa wa kampuni hiyo kuelezwa na kufafanua kwa kina kuhusua faida za kununua hisa hizo.
Akizungumza na wananchi wa Mbezi Mwisho ,Ofisa wa Kampuni ya JATU PLC Mohamed Simbano amesema mkakati wa kampuni yao ni kuhakikisha inashiriki kuwaokomboa wananchi wa Dar es Salaam kiuchumi, hivyo imeamua kuja na mfumo huo wa ununuzi wa hisa kama dhamana ya kuendeleza kwa faida shughuli zao za kiuchumi.
"Hisa moja iauzwa Sh.500 na mteja ili aweze kujinga nasi anatakiwa kununua hisa 10, hivyo atatakiwa kuwa na Sh.5000.Tangu tumeanza kampeni hii ya kuuza hisa za JATU ili kuwoakomboa wananchi kiuchumi, muamko mmekuwa mkubwa, watu wananunua hisa zetu sana,"amesema.
Baada ya kupatiwa elimu kuhusu faida za hisa za JATU PLC , wananchi wa Mbezi Mwisho na Mabibo mkoani Dar es Salaam wametoa pongezi kwa kampuni hiyo kwa jitihada zake za kuwainua kiuchumi .Wamesisitiza wataendelea kununua hisa hizo kwa faida zake ni nyingi na hasa kwa kuzingatia wengi wanaonunua ni wale ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Amina Bakari na John Mathias ambao wanaishi Mbezi Mwisho wamesema wanatambua hivi sasa kila mwananchi amekuwa akijisghulisha na utafutaji fedha kwa kufanya biashara mbalimbali, hivyo JATU imekuja kwa ajili ya kuwaongezea nguvu na hatimaye kujikomboa kiuchumi kwa kuimarisha mitaji yao kifedha kupitia hisa za kampuni hizo.
Wakati Andrew Masunga na Jafari Mpenda ambao ni wakazi wa Mabibo wao wamesema kuwa mwanzoni walikuwa wakisikia tu kuhusu JATU lakini baada ya kupata elimu kuhusu hisa hizo wameamua nao kujiunga kwa kununua ili kuwa sehemu ya wanufaika.
Wameongeza kuwa Kampuni ya JATU PLC imewafanya wananchi wa Mabibo kuwa na mtazamo nyanya wa kushiriki kikamilifu kwenye kuleta maendeleo na watafikia malengo kwa kununua hisa za kampuni hiyo.
Dereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Gongolamboto na Mbezi Mwisho Said Kindamba ametumia nafasi hiyo naye kuelezea furaha aliyonayo baada ya kununua hisa za kampuni hiyo na kwamba mbali ya kuwa dereva lakini anajishughulisha na ujasiriamali mdogo mdogo, hivyo anakwenda kuongeza mtaji wake kupitia hisa za JATU PLC.
No comments: