WATANZANIA WATAKIWA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA
WATANZANIA kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, wametakiwa kuendelea kumpongeza kwa kuendelea kusimamia Uhuru, Amani, Umoja na Mshikamano wa Taifa.
Pongezi hizo zilitolewa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Charles Sabiniani maarufu kama (Lowassa) wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana.
Lowasa ambaye pia ni Meneja Miradi wa Taasisi ya Maendeleo ya Pikipiki na bajaji alisema watanzania wanatakiwa kumuunga mkono Mama aliyetabiriwa kuongoza Taifa.
Lowasa alisema kuwa alitembelea makumbusho ya Kaole yaliyopo Bagamoyo na kujionea mambo mbalimbali yenye kuakisi hali ya sasa.
"Nilitembelea makumbusho ya kaole, lengo likiwa nikufika kwenye kaburi la sharifu binti ambaye alikua na maono mengi pia watu wengi miaka hiyo walimuona kama binti na mwanamke wa pekee alitabiri kifo chake," alisema Lowasa na kuongeza,
"Ukisikiliza zaidi historia yake alitabiri kuwa mwanamke atakuja kuongoza lakini nipende kusema kuwa pamoja na historia hii nimefika pia kama kada na mtoto wa marehemu willibadius aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na kada mtiifu naMnimefika kumwombea baraka Mama yetu Samia mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa Rais naamini uongozi wake utakua na baraka kubwa kwa imani," alisema.
Aidha alitoa wito kwa vijana, akina mama na akina baba kupenda kutembelea makumbusho na kusema''ukitembelea makumbusho unajifunza vitu vingi sana na unapata ujasiri kwani pale nimeona mwaka 1480 watu wanapambana na kusaka pesa hivyo nimeamini kauli ya Hayati John PombeMagufuli ya hapa kazi tu pamoja na Mama yetu Samia kazi inaendelea ," Alisema.
Mbali na hilo Meneja Lowasa wakati wa mkutano wa madereva wa pikipiki na bodaboda ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa Taasisi hiyo Rose Mkisi alisema ni wakati muafaka kwa vijana kuelekeza matumaini yao kwa Rais Samia.
Naye Mjumbe huyo wa bodi aliwahimiza madereva hao kuendelea kufanya kazi zao kwa uaminifu huku akiahidi kuchangia kiasi kadhaa cha fedha kwa Taasisi hiyo.
No comments: