WASHIRIKI MISS DODOMA WAPATIWA ELIMU YA KUJITAMBUA,VVU NA UKIMWI
Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WANAOSHIRIKI katika Mashindano ya Urembo wametatakiwa kutumia nafasi yao kwa ajili ya kuisaidia jamii hasa vijana.
Akizungumza na Michuzi Tv Ezekiel Kwakwa ambae ni Afisa uhusiano wa Shindano la Miss Dodoma katika Mkutano wa mwaka wa Wadau wanaotekeleza Afua za vvu na ukimwi zinazolenga Wasichana balehe ,wanawake pamoja na Vijana amesema ni nafasi nzuri kwa Washiriki hao kupatiwa kwani imewapa fursa ya kujitambua na kujua nafasi yao katika jamii .
Aidha, Amesema lengo na dhumuni la kuhudhuria Mkutano huo ni kuwaandaa Wasichana hao ambao baadae watakua viongozi na wawakilishi wazuri kwenye jamii kutokana na nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa Wasichana wenzao kuanzia mashuleni,mitaani na sehemu mbalimbali.
"Ni fursa ya kipekee kwa Washiriki hao kupatiwa elimu ambayo itawanufaisha na kuitumia kwa jamii ili kuona kwa namna gani tunapunguza Kasi ya Magonjwa Kama vvu na kuona kwa namna gani vijana wanaweza kuepuka Vishawishi vya ngono ."
Pia ametolea ufafanuzi swala la urembo kuonekana Kama uhuni kwenye jamii kutokana na baadhi ya Warembo kujihusisha na skendo mbalimbali ambazo hupelekea Sekta hiyo ya urembo kuonekana Kama Haina heshima kwenye jamii.
"Urembo ni heshima kutokana na baadhi ya Viongozi Serikalini wamepita kwenye mikono ya urembo hasa Miss mfano mzuri Jokate Mwegelo,Flavian Matata na wengine wengi hivyo Urembo sio uhuni ni kazi pia ni mfumo ambao husaidia kukuza wengine na baadae kusaidia jamii na ndio maana licha ya kuwa Miss Dodoma mrembo pia anapata fursa ya kutengeneza kitu ambacho kitasaidia jamii yani Mpango kazi."
Kamati na Washiriki wa Shindano la Miss Dodoma wakiwa na Mwanamitindo Flavian Matata pamoja na Mkurugenzi na Muandaaji wa Shindano Hilo Alexander Nikita kwenye Mkutano wa mwaka wa Wadau wanaotekeleza Afua za vvu na ukimwi zinazolenga Wasichana balehe wanawake pamoja na Vijana jijini Dodoma.
No comments: