WANANCHI ARUMERU KUONDOKANA NA ADHA YA MAJI

Jane Edward Michuzi TV, Arusha

Wananchi wilayani Arumeru Mkoani Arusha wanatarajiwa kuondokana na adha ya maji ,baada ya Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Noah Lemburis Saputu kukabidhi mipira ya maji kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji zenye dhamani ya takribani shs 10 milioni .

Aidha mipira hiyo imekabidhiwa katika Kijiji cha Mzimuni kilichopo kata ya Nduruma na kijiji cha Sasi kilichopo kata ya Bangata wilayani Arumeru .

Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo,Mbunge huyo alisema kuwa,vijiji hivyo vimekuwa vikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Maji kwa muda mrefu ambapo wananchi wake wamekuwa wakipata adha kubwa ya kuamka usiku kufuata maji umbali mrefu.

Alisema kuwa,mradi huo wa maji katika kijiji cha Mzimuni unatoka katika kata Mlangarini , ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa mipira hiyo kwa ajili ya kupeleka maji kijijini hapo.

Diwani wa kata ya Nduruma ,Raymond Mollel alisema kuwa,wanamshukuru Sana Mbunge kwa kuwaletea mipira hiyo ya maji kwani kwa Sasa changamoto ya maji katika Kijiji hicho itakuwa imeisha kabisa.

Nao baadhi ya wananchi wakizungumzia mradi huo,Saiguran Mollel alisema kuwa,anashukuru Sana kwa kitendo Cha Mbunge wao kuanza kutimiza ahadi alizotoa katika kata hiyo ikiwemo kutatua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wa muda mrefu .

Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Noah Lemburis Saputu akikabidhi mipira ya maji kwa diwani kata ya Nduruma (Picha na Jane Edward Michuzi TV, Arusha)

No comments: