WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI 409 MKOA WA MARA WAPATA MAFUNZO JUU YA NAMNA BORA YA UCHUKUAJI WA SAMPULI WAKILISHI NA UCHENJUAJI BORA WA MADINI
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika mpango wake wa kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini leo tarehe 18/5/2021 imefanikiwa kutoa mafunzo Kwa wachimbaji 409 katika Mkoa wa Mara kwa kipindi cha siku tatu.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa tarehe 16/5/2021 na mheshimiwa Waziri wa Madini Doto Biteko yamefanyika kwa nadhari na vitendo katika sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mara ambapo jumla ya wachimbaji wadogo wa Madini 270 walipata mafunzo Kwa vitendo ambapo eneo la Buhemba wachimbaji wadogo 37 , Gedeli wachimbaji 126,Nyamongo wachimbaji 67, Ikungu wachimbaji 40 , Kwa upande wa nadharia jumla ya wachimbaji 139 walifundishwa.
No comments: