TBL YASHIRIKI KUENDELEZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KUTUNZA MAZINGIRA NA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI
Na,Jusline Marco;Arusha
Kampuni ya TBL Plant ya Arusha imeonyesha ushiriki wake kwenye zoezi la upandaji miti na usafi wa mazingira katika vyanzo vya maji na pembezoni mwa mito ikiwa ni uungaji mkono juhudi za kuendeleza wa kampeni ya upandaji miti kwa ajili ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji jijini Arusha.
Mdau wa mazingira ambaye pia ni Meneja Mauzo kutoka katika kampuni hiyo,Bwn.Joseph Raymond Mwaikasu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo alisema kauli mbui waliyonayo katika utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni muhimu kwao katika kuendeleza harakati za utunzaji wa vyanzo vya maji na mito.
Mwaikasu aliongeza kuwa kama kampuni wanashirikiana jamii kuweza kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili viweze kuendelea kuwasaidia katika uzalishaji na hata jamii inayowazunguka hivyo kama kampuni wana sehemu kubwa kuweza kuwajibika katika masuala ya kijamii.
"Tumekuwa wadau na Bonde la Pangani na kushiriki katika matukio mbalimbali na tumetoa mabango yenye ilani lwa kutoa tahadhari kwa wananchi katika ile mipaka ya vyanzo vya maji ambapo mabango haya tumeyaweka katika mto Themi pamoja na Mto Ngarenaro."Alisema Mwaikasu
Sambamba na hayo alisema kuwa katika ushiriki wao wametoa vipeperushi zaidi ya elfu nne(4000) ambavyo vinaonyesha ujumbe muhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na usafi katika mito ili kuhakikisha maeneo yote ya maji yanatunzwa na na kulinda vyanzo vya maji ikiwa nimoja ya vipaumbele vya kampuni hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani Injinia Segule Segule alisema kuwa katika utunzaki w a vyanzo vya maji muitikio wa wananchi umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa mwanzoni kwani watu wamekuwa wakiachakufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya maji.
"Hii ni kiashirio tosha kuwa watu wa jamii nzima imepata uelewa wa namna vyanzo vya maji vinapaswa kutunzwa bola kuangalia tofauti za kiumri na kielimu,leo hapa tuna watu wa kawaida kabisa mpaka maofisa wakubwa wa serikalini."Alisema Injini Segule
Aliongeza kuwa hali ya vyanzo vya maji kwa sasa inaendelea kuwa bora kutokana na kampeni zinazoendelea na misimamo ya serikali uliyopo wa kuweka nguvu katika maeneo yote hali inayosababisha uoto wa asili kwenye maeneo mbalimbali unarudi.
Vilevile alisema kuwa mikakati ya Bodi ya maji Bonde la Pangani kuendelea kuwatoa baadhi ya watu waliobaki katika hifadhi za maji watachukuliwa hatua mbalimbali kwani suala la utambuzi tayari lilishafanyika na kifahamu kama watu hak walifuata vyanzo vya maji au vyanzo hivyo ndivyo viliwafuata ambapo jitihada zankuhamasishana katika maeneo ya namna hiyo zimeanza.
"Tumeanza kuhamasishana kwa wananchi ambao wapo katika hifadhi za maji ambao mito imewafuata sambamba na kuwaondoa wale ambao wapo katika maeneo hatarishi zaidi kwa usalama wa mito ambapo zaezi hili linaenda taratibu kulinganana upatikanaji wa rasilimali wa nanmna ya kulitekeleza."Alisisitiza Segule
Pamoja na hayo aliwataka wananchi kuzingatia sheria na kuweza kukaa nje ya eneo la hifadhi ya mito ili kuweza kulinda vyanzo hivyo sambamba na kuepuka madhara ya mafuriko ambayo kwa namna moja ama nuingine yanaweza kutokea.
Akizindua kampeni hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maxmilian Iranghe amesema kuwa lengo la jiji la Arusha ni kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ili viweze kuwa endelevu ambapo amewataka wananchi,wadau mbalimbali ikiwemo watu wa utalii kuungana pamoja na kuifanya Arusha kuwa ya kijani.
"Vyanzo hivi vya maji tunatakiwa tuhakikishe tunavitunza ili viweze kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo viweze kunufaika."Alisema Meya huyo
"Hapa tuna zoezi la kupanda miti na miti mara nyingi ni chazo cha kuhifadhi maji,tukikata miti maji yanapotea hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anapanda miti katika vyanzo vya maji sambamba na kutunza vyanzo hivyo."Alisisitiza
Aliongeza kwa kusema milango ya jiji la Arusha ipo wazi kwa zaoezi la upandaji miti kwa ajili ya kuendelea kuifanya Arusha iwe ya kijani ambapo aliwaomba wadau mbalimbali wa mazingira wakiwemo watu wa utalii kuwawezesha miche ya miti ili kuweza kuiotesha sehemu mvalimbali ndani ya jiji la Arusha ambapo tayari halmashauri ya jiji hilo imetoa miche ya miti ipatayo Laki moja na Ishirini (120000) kwa kipindi cha mwaka huu huku kipaumbele kikubwa kikiwa ni vyanzo vya mito.
Vilevile Meya huyo aliwaomba wananchi wa jiji la Arusha kutoa ushirikiano katika zoezi la upandaji miti klu kuweza kuhifadhi vyanzo vya maji huku wakifahamu kuwa jukumu la kuifanya Arusha kuwa ya kijani nj jukumu la kila mmoja sambamba na kuhakikisha vyanzo vya maji vinakuwa safi wakati wote na zoezi hilo kuwa endelevu.
"Jiji la Arusha tuna mito mingi ikiwemo mto Naura,Themi,Ngarenaro,Kijenge pamoja na Oreresho yote kwa pamoja tunapaswa kuhakikisha kuwa inabaki kuwa misafi ili iweze kutumika kama kivutio vya utalii kwa sababu utalii unaanza na sisi wenyewe."Aliongeza Mstahiki Meya
Awali akimwakilisha Mkurugenzi wa jiji la Arusha,James Lobikoki amesema kuwa lampeni hiyo itaweza kuondoa changamoto ya uvamizi wa shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.
Meya wa Jiji la Arusha Maxmilian Iranghe akishirikiana na wananchi katika usafishaji wa Mto Ngarenaro.
Meneja Mauzo kutoka katika kampuni ya TBL Plant ya Arusha,Bwn.Joseph Raymond Mwaikasu akifanya usafi katika Mto Ngarenaro kwenye uzunduzi wa Kampeni ya upandaji miti kwa ajili ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji jijini Arusha.
No comments: