SHAKA AWAKUMBUSHA WANANCHI KWA UJUMLA KUENDELEA KUCHAPA KAZI, ASHIRIKI SWALA YA EID AL- FITR UJIJI MKOANI KIGOMA
Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka amewahimiza wananchi wote kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuzalisha ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa, sambamba na kutimiza kutunza na kuimarisha hali ya amani, utulivu, umoja na Mshikamano katika nchi yetu.
Amesema hayo leo baada ya kumalizika kwa swala ya Eid Al- Fitr mbapo Shaka aliungana na waumini wa Dini ya Kiislam Mkoa wa Kigoma kushiriki swala hiyo iliyosaliwa katika Uwanja wa Stendi Mpya ya Ujiji-Kigoma mapema leo tarehe 14 Mei 2021.
Swala hiyo iliyoongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Sheikh Hassan Kiburwa ilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wa zalendo Ndugu Juma Duni Hajji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ndugu Suleiman Jafo.
Pia, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Kilumbe Shaban Ng'enda, Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hillary na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Ndugu Maryam Ditopile.
Katika salamu zake za Eid Al-Fitr kwa waumini wakati wa Swala, Mwenezi Shaka amefikisha salamu za Eid kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, ambapo amewaambia waumini kuwa;
"Mwenyekiti wetu na Rais wenu mpendwa amenituma niwaeleze kuwa anawapenda na anawatakia heri na furaha katika siku muhimu duniani"
Amewaomba waumini kuliombea Taifa pamoja na kumuomba MwenyeziMungu amjaalie Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan, ampe Afya njema, maono na msimamo thabiti katika kuiongoza nchi yetu.
Aidha amesisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi wote kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kuzalisha ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa, sambamba na kutimiza kutunza na kuimarisha hali ya amani, utulivu, umoja na Mshikamano katika nchi yetu.
No comments: