Serikali yaanika nafasi za nyongeza kujiunga na jeshi la kujenga taifa (JKT)




Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi,Ruth Msafiri amesema jeshi la kujenga Taifa (JKT) katika mwaka wa 2020/2021 limetoa nafasi za nyongeza kwa vijana waliohitimu darasa la saba na kidato cha nne tu,kujiunga na mafunzo kwa mkataba wa miaka miwili kwa utaratibu wa kujitolea na maombi hayo yakianza kupokelewa hii leo mpaka hapo kesho Mei 6,2021.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwakwe huku akitoa wito kwa vijana wanao hitaji na wenye sifa za kujiunga na jeshi hilo kufuata utaratibu ili waweze kujiunga kupitia nafasi hizo.

“Sifa ni zile zile za siku zote kwanza ni lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 16-18 kwa vijana wenye elimu ya darasa la saba,huku vijana wenye elimu ya kidato cha nne awe na umri usio zidi miaka 20”Alisema Ruth Msafiri

Amesema sifa zingine ni pamoja na “Awe na afya njema,akili timamu na asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo),vile vile awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri na hajapatikana na hatia mahakamani wala kuwahi kufungwa”alisema Msafiri

Kuhusu uafaulu wa kijana anayehitaji kujiunga na jeshi hilo mkuu wa wilaya amesema. “Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari safari hii wamekuja na uafaulu,kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2018,2019 na 2020 wenye ufaulu wa daraja la tatu na la nne (Div.111 na Div 1V) na hawajatuambia poit”alisema Ruth Msafiri

Hata hivyo amesema ni muhimu vijana hao kuwa na uthibitisho wa kuhitimu elimu ya msingi pamoja na cheti halisi cha kuzaliwa huku wale waliomaliza kidato cha nne ni muhimu kuwa na cheti halisi cha kumaliza shule.

Vile vile Msafiri amesema nafasi hizo na kwa vijana wasio wahi kutumikia jeshi la polisi

“Awe hajawahi kutumika jeshi lolote liwe jeshi la polisi,Magereza,chuo cha mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na idara nyingine serikalini na asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma kwasababu kuna wengine wakiskia nafasi wanarudi tena”alisema Msafiri.

Amesema barua za maombi hay ohayo zinapaswa kupitishwa kwa maafisa watendaji wa kata au kijiji husika anapoishi mwombaji ili kuthibitisha ukaazi wake huku zikiwa zimeambatanishwa na vivuli vya vyeti vinavyohusika katika maombi na kuwataka viajana kuchangamkia fursa hiyo inayotarajia kuanza usaili Mei 7 mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akitangaza nafasi hizo za nyongeza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo.

No comments: