SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI PAMOJA NAKUWALINDA

Na.Vero Ignatus,Arusha.

SERIKALI imeahidi kushirikiana na waandishi wa Habari wote nchini katika shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwa ni Pamoja na kuwalinda waandishi wa Habari na kulinda haki zao.

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya kuelekea siku ya Redio duniani.

Sambamba na hayo Kihongosi ametoa wito kwa waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri kwa kuandika Habari ambazo zitawaunganisha watu na kuleta maendeleo ya kiuchumi hususan katika nchi za Africa mashariki na kwamba kalamu inaweza kujenga au kubomoa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Peter Mathuki ameitaka jamii kutambua umuhimu wa waandishi wa Habari na amelishukuru shirika la UNESCO kwa kuandaa maadhimisho hayo na kutoa wito kwa waandishi kuwajibika na kuandika Habari ambazo zitaleta watu Pamoja na kukuza maendeleo ya kiuchumi ulimwenguni.

Akitoa salamu za shukrani Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Arusha (APC) Claud Gwandu amewashukuru Freedom House kwa kufanikisha maadhimisho hayo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza mara kwa mara kunapokuwa na matukio ya kihabari kama haya.

Siku ya Redio duniani ilianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa ajili ya kusherehekea matangazo ya redio, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa miongoni mwa watangazaji wa redio na hufanyika kila Ifikapo tarehe 3 ya mwezi wa tano ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni Habari kwa manufaa ya Umma.

Waandishi wa habari kutoka katika mikoa mbalimbali wakiwa katika mazoezi ya viungo katika uwanja wa shekhe Amri Abeid mkoani Arusha

No comments: