SERIKALI MBIONI KUTUNGA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa washiriki wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikitoa semina kwa wabunge kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti Kulia ni Naibu Spika wa Bunge. Dkt. Tulia Ackson na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso ,Semina hiyo imefanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akifunga kikao cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania baada ya kuwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe akiwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile iliyofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe (hayupo pichani) kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge .Anayefuata ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Wizara hiyo, Elisa Mbise kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabri Kuwe (hayupo pichani) kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma wakati wa Semina kwa wabunge yenye lengo la kujua huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake
Dkt.Ndugulile amesema kuwa tayari wizara imeshaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo.
Hata hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa
“Mkiangalia kwa sasa uharamia na ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesema Dkt. Ndugulile
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali kuongeza fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote pamoja na kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani
Naye Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson ametoa pongezi kwa Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
No comments: