RAIS WA ZANZIBAR DK.MWINYI ATOA MKONO WA EID EL FITRY KWA WANANCHI WALIOFIKA IKULU JIJINI ZANZIBAR.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumaliza kuzungumza na baadhi ya Masheikh wa Zanzibar waliofika Ikulu Jijini Zanzibar kumsalimia na (kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na baadhi ya Masheikh waliofika Ikulu Jijini Zanzibar kumsalimia, baada ya kutoka katika Sala ya Eid El Fitry, iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi waliofika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumsalimia na kupokea mkono wa Eid El fitry.(Picha na Ikulu)

No comments: