RAIS SAMIA ATAKA MFUMO MMOJA KUTAMBUA MADEREVA WANAOFANYA MAKOSA BARABARANI, WIZI MTANDAONI WAMKERA ...AHOJI USAJILI LINI KWA VIDOLE
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
JESHI la Polisi nchini limeshauriwa kuanzisha mfumo wa kieletriniki ambao utasomeka nchi nzima ili dereva akifanya kosa eneo moja basi liingizwe kwenye mfumo huo na lisomeke kwa nchi nzima na baada ya kusomeka ndipo aidha atozwe faini na akikosa tena zaidi ya mara tatu au nne aingizwe kwenye orodha ambayo anaweza akanyang’wanywa leseni.
Ushauri huo umetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua Kiwanda cha Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam ambapo amesema kumuwekupo na makosa yanayofanywa na baadhi ya madereva,hivyo labda mfumo huo ukianzishwa na wanaofanya makosa mara kwa mara wakanyang'anywa leseni huenda ikaleta heshima.
"Dereva akikosea na makosa yakifika matatu au manne ananyang’anywa leseni labda hii kidogo italeta heshima lakini kwasababu akifanya Dar es Salaam ,kesho anakwenda kufanya kosa Morogoro na kesho kutwa Dodoma na makosa hayasomani wanaendelea kufanya makosa, hivyo niwaombe muweke mfumo huu ili muweze kudhibiti ajali za barabarani.
Wakati huo huo,Rais Samia amesema mbali na makosa hayo ya barabarani, jeshi hilo limezungumzia kuhusu kuongezewa uwezo kwenye masuala ya sayansi na teknolojia . " Hilo nijambo muhimu sana na kama mnavyofahamu kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia makosa mapya yamejitokeza yawekimo ya wizi wa mtandao.
"Na hapa nataka niseme ukweli kwamba kuna mambo huwa yanatushangaza, kwa mfano mtakumbuka kulikuwa na sheria wote tufanye usajili wa namba zetu za simu na mambo yote ili ijulikane mtu anayetumia hiyo namba lakini pamoja na usajili huo vitendo vya utapeli kupitia mitandano babo unaendelea na unashamiri.
"Hatusikii watu wamefikishwa mahakamni kwa ajili hiyo , najiuliza ule usajili ulikuwa kiini macho au ni nini? Kama tulisajili kila mtu awe anajulikana na kama kuna namba hazijulikani zinatolewa na shirika gani ?Naomba msimamie hilo mkishirikiana na taasisi ya mtandao wa serikali.
"TCRA na taasisi nyingine za fedha za umma na binafsi yakiwemo mabenki na kampuni za simu kwa ajili ya kushushughulikia suala hilo , wizi wa kimtandao uwe unafanywa ndani au unaovuka mipaka naomba yasimamiwe,"amesema Rais Samia.
No comments: