MFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO 400 ZA DAWA ZA KULEVYA
Mfanyabiashara Frank Mwita akiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu leo Mkoani Dar es Salaam kusomewa mashtaka yanayomkabiri.
MFANYABIASHARA, Frank Mwita anayeishi Dar es Salaam amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kukutwa na zaidi ya kilo 400 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando imedai, Februari 25, mwaka huu huko katika kijiji cha wavuvi Kurasini ndani ya Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam mshtakiwa alikutwa akiwa na kilo 446.11 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 3, 2021 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa mshtakiwa amerudishwa rumande.
No comments: