MBUNGE KUNAMBI AITAKA WIZARA YA UJENZI KUAGIZA TAZARA KUJENGA KITUO KIDOGO CHA TRENI KATA YA CHISANO
Charles James, Michuzi TV
MBUNGE wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi ameipongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mpango wake wa kuifanyia upembuzi yakinifu wa Kilomita 220 Barabara ya Morogoro-Njombe Boda huku akiomba kuharakisha mpango huo ili kuleta neema kwa wananchi wake wa Jimbo la Mlimba.
Kunambi ameyasema hayo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya Wizara hiyo ambapo amesema kuhusu upembuzi yakinifu wa Barabara hiyo ya Kihansi Mlimba Taweta Madeke tangazo la kutafuta mkandarasi mshauri wa kujenga barabara hiyo lilifanyika miezi mitatu iliyopita na hivyo kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk Leonard Chamurilo kueleza ni lini kazi hiyo ya upembuzi yakinifu itaanza.
Kunambi amesema wananchi wa Jimbo lake ni watumiaji wakubwa wa Reli ya Tazara na hapo awali ilikua na vituo vidogo vya abiria wanaosafiri kusimama kusubiri Treni lakini baadhi yao vimekufa na hivyo kuwapa tabu wananchi hao.
“ Wananchi wangu wa Mlimba ni wadau wakubwa wa Reli ya Tazara kwa sababu ni wafanyabiashara sasa kulikua na vituo vidogo vya abiria kusubiri treni vinaitwa Hot stesheni sasa kulikua na hot stesheni ya kata ya Chisano lakini kwa muda mrefu imekua haifanyi kazi hivyo nikuombe Waziri uagize kituo hiki kidogo kianze kazi.
Waziri nakuomba uagize kituo hiki kidogo kianze kazi ili kupunguza adha ya kunyeeshewa na mvua au kupigwa na jua inayowakumba wananchi wangu kwa kusubiri Treni, na hawa watu ni wafanyabiashara hivyo ni vema Wizara muelekeze Tazara wajenge vituo hivi, tofauti na hapo Waziri nitashikilia Shilingi yako,” Amesema Kunambi.
No comments: