MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA BALOZI BRIG. JENERALI IBUGE NA BALOZI JOSEPH SOKOINE
Na Mwandishi wetu, Dar
ALIYEKUWA Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Joseph Edward Sokoine.
Makabidhiano ya ofisi yameshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb).
Aliyekuwa Katibu Mkuu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya Balozi Joseph Sokoine. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberat Mulamula (Mb) akimkabidhi ua Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam kwa makabidhiano ya Ofisi. Kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
No comments: