LOWASA ACHANGIA MILION 11 UJENZI WA NYUMBA YA DAKTARI

Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa amechangia Sh milioni 11 katika miradi ya maendeleo kwa  vijiji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya daktari wa wilaya hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake kwa wapiga kura wa jimbo la  Monduli.

Taarifa ya Ofisi ya Mbunge huyo kwa vyombo vya habari, imesema fedha hizo ni kutokana na mchango wa Mbunge aliyetoa zaidi ya Sh milion 6.8 na taasisi ya ECLAT DC iliyotoa Sh milioni  5.

Fredrick ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametoa mchango huo jana alipotembelea eneo litakalojengwa nyumba ya daktari wa wilaya.

Pia Lowasa ameweza kutembelea  eneo la shule ya Msingi ya Endonyonaado iliyoezuliwa paa lake na upepo, pamoja na zahanati  ya Kata iliyopo Engutoto kijiji cha Mlimani.

Lowassa amewashukuru wananchi kwa kumchagua kwa asilimia 93 yeye pamoja na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk John Magufuli.

“Ninawashukuru sana  kwa kutuchagua kwa asilimia kubwa mimi pamoja Hayati Magufuli, licha ya kutokea  msiba mkubwa wa kitaifa na kumpoteza  sasa tunaye  Rais Mama Samia Suluhu Hassan,” amenukuliwa Lowassa akisema katika taarifa hiyo.

Lowassa aliyebeba kauli mbiu ya baba yake ya Elimu Elimu Elimu, alimuomba mfadhili huyo kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na Ofisi ya Mkurugenzi kusaidia kujenga Shule ya Msingi Endonyonaado ambacho wananchi walijenga madarasa mawili na kupauwa lakini upepo uliezua.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima  alimshukuru Lowassa kwa kumkaribisha jimboni kwake na kuahidi kumuunga mkono katika shughuli za maendeleo.
Taarifa hiyo imesema Lowassa alifahamiana na taasisi hiyo baada ya kutembelea makao kakuu yake yaliyopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara na ndipo alipowaalika.

“Kwa heshima hiyo na umuhimu wake alionionyesha Mbunge wa Jimbo la Monduli ninamuahidi kumuunga mkono wa dhati,  Mbunge naomba nikajiandae kwa kazi hiyo na niaahidi mwezi wa saba ikimpendeza Mwenyenzi Mungu nakuja na wafadhili eneo hili la Indonyonaado,” amenukuliwa akisema Toima katika taarifa hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa akijadili jambo na Mkurugenzi  wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima walipotembelea vijiji vitakavyonufaika na ujenzi wa nyumba ya daktari na kuchangia kiasi cha Sh Milion 11
Mkurugenzi  wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima akizungumza na wananchi wa Jimbo la Monduli baada ya kuchangia kiasi cha Milion 5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya daktari
Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa akiwa  na Mkurugenzi  wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima walipotembelea vijiji vitakavyonufaika na ujenzi wa nyumba ya daktari na kuchangia kiasi cha Sh Milion 11
 

No comments: