LHRC, TAVICO waliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji ya kikatili

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mauaji ya kikatili kwa mtoto mwenye Ualbino mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Godson Mollel akizungumza kuhusiana namna Chama kinavyolaani mauji ya watu wenye Ualbino,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji wa Shirika la Tabora Vision Community Based (Tavico) Focus Magwesela wa kwanza kushoto akizungumza kuhusiana namna alivyopata taarifa na kufatilia tukio la mtoto mwenye Ualbino  ,jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Maduhu William akizungumza kuhusiana na tukio la mauaji  ya kikatili ya mtoto mwenye Ualbino ,jijini Dar es Salaam.

*Ni Mtoto Mwenye Ualbino, baadhi ya viungo vilitolewa ni mikono miwili,Macho na Sehemu za Siri.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wake kutoka Shirika la Tabotlra Vision Community Based (Tavico) limeiomba Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi wa Mtoto mwenye Ualbino anayekadiliwa kuwa na umri Kati ya miaka mitano hadi sita aliyeuawa kikatili Mkoani Tabora.

Tukio hilo lilitokea kati ya Mei 3 na 4 mwaka 2021 baada ya kukuta mwili ikiwa umelekezwa kwenye majani karibu na dimbwi la maji katika kitongoji cha Usadala kilichopo Kijiji cha Utemini kata ya Ndono Wilayani Uyui mkoani Tabora.

Mwili wa Mtoto mwenye Ualbino huyo uliokotwa na wanakijiji ukiwa umekatwa sehemu za siri,Mikono pamoja na kutolewa macho.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga amesema kuwa hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kuhusiana na unasaba na mtoto huyo.

Amesema licha ya kuwa mtoto mwenye Ualbino Binadamu wote wamezaliwa hivyo kunahitaji uchunguzi wa kina kujua alitolewa wapi pamoja na wahusika waliofanya tukio hilo wakawekwa katika mikono ya sheria.

Henga amesema kuwa timu LHRC na Tavico wamefanya ufatiliaji wa kujua mtoto huyo pamoja na vituo na kuambiwa wako salama.

Aidha amesema kuwa wana imani na Jeshi la Polisi wanaweza kufanya uchunguzi kwa mbinu zao na kujua mtoto alitolewa wapi pamoja na kujua wazazi wake.

Amesema taarifa hizo zilitolewa kituo cha Polisi Wilaya ya Uyui siku hiyo hiyo majira ya sita hadi saa Saba Polisi walifika kwenye eneo majira ya saa tisa mchana na kisha kuukagua mwili marehemu ikiwa ni pamoja na kupiga picha.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Tavico Focus Magwesela amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi kulichukulia Jambo la mauaji hilo kwa umuhimu wa hali juu kama anavyofanya kwenye mambo mengine ya kiuhalifu hapa nchini.

Amesema kuwa wanaiomba Serikali kuhakikisha taarifa za tukio hilo kutoka kwa Mamlaka zinawekwa wazi kwa umma na kuonyesha njia ambayo inaweza kutumiwa na wazazi au walezi wa marehemu kupata taarifa sahihi za mahali alipozikwa ndugu zao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Godson Mollel amesema wanalaani tukio hilo na kuomba vyombo vya serikali kulifanyia kazi.

Kwa upande wa Mwanasheria Maduhu William amesema walikwenda Tabora na kuona hali hiyo na kuongeza kuwa licha ya kuwepo tukio hilo lakini hakuna taarifa yeyote hadi Sasa kwa Mamlaka za Serikali kuzungumzia.

No comments: