KAWEJURU FELIX (CCM) ASHINDA UBUNGE JIMBO LA BUHIGWE

 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Marycelina Mbehoma akikabidhi Cheti cha ushindi mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma, Kavejuru  Felix   wa Chama cha Mapinduzi baada ya kuibuka mshindi na kuwabwaga wapinzani wake 12 alioshiriki nao katika Uchaguzi mdogo uliofanyika Mei 16,2021. Mgombea huyo alipata kura 25,274 Kati ya kura 30,320 ya kura halali zilizopigwa.

Mgombea wa ACT Wazalendo Garula Kudra alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 4,749 na nafasi ya tatu ikienda kwa Abdallah Bukuku wa Chama cha CHAUMA aliyepata kura 125.

No comments: