CCM YASEMA WAPINZANI KUSHINDWA NI LAZIMA MAJIMBO YA BUHIGWE, MUHAMBWE
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka ameufananisha uchaguzi mdogo wa majimbo ya Muhambwe na Buhigwe kama vita vya Kagera vilivyomgaragaza na kumuondoa Nduli Idd Amin Dada na majeshi yake ndani ya mipaka ya Tanzania mwaka 1978/1979 .
Amesema ni lazima adui apigwe bila huruma na kuhakikisha majeshi yao yanafukuzwa hadi nje ya karibu na mipaka ya DR Congo.
Shaka ameeleza hayo alipokuwa akitumia lugha ya kifasihi katika uzinduzi wa mkutano wa hadhara wa kampeni huko Kibondo mkoani Kigoma hapa mbele ya mgeni rasmi Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Majaliwa Kasim Majaliwa.
Amesema mwaka 1978 nchi yetu ilivamiwa na majeshi ya Uganda tukalazimika kuyachakaza. Kipigo kama kile kitawapata tena watani wao Muhambwe na Buhingwe.
Amesema sababu ya watani kupigwa watani zipi nia na uwezo wa kuwatandika upo hivyo kazi iliobaki ni moja tu ya kuwashinda kwenye chaguzi zote mbili kwenye majimbo hayo.
" Chama kimeweka dago Muhambwe na Buhigwe kuhakikisha tunashinda kwa haki, amani na kwa ushindani wa kidemokrasia .CCM ni waumini wa demokrasia shirikishi . Tumeshaingia kwenye uwanja wa mapambano hatutarudi nyuma hadi ushindi utakapopatikana,, "amesisitiza Shaka
Ameongeza katika uchaguzi huo watashinda kwa mbinu za matumizi ya sera na sayansi ya siasa hatimaye kuwaacha mbali washindani wao kwani baadhi ya vyama vinashiriki uchaguzi huu kwa lengo la kusindikiza Chama Cha Mapinduzi na wagombea wake.
"Tumebeba baadhi ya mitambo muhimu inayoweza kupiga katika masafa mafupi na marefu .Kazi ilio mbele yetu ni kuwatandika bila huruma watani wetu ili kuwafundisha nidhamu ya siasa ,maana ya uchaguzi na CCM kilivyo makini" amesema.
Aidha amesema kwamba kwa Katiba ya Chama hicho wamefanya vikao vyake kuanzia ngazi za chini hadi juu vya kuyapitisha majina ya wagombea walioingia kuwa sifa na walioshiriki kwenye mchakato huo wanaendelea kutoa ushirikiano kwa wenzao.
"CCM si chama cha nongwa au mizengwe au kuwekeana mifundo na vinyongo. Uchaguzi ndani ya chama unapomalizika kila mwanachama hutakiwa kuheshimu maamuzi. Jeshi letu ni moja hivyo kila askari hutakiwa kwenda mstari wa mbele,"amesema Shaka.
No comments: