BROTHERS TO MEN WAIPIGA JEKI SHULE YA MSINGI JANGWANI


Mwenyekiti wa Kikundi cha Maendeleo ya Jamii Brothers To Men Paul Kivumbi akimkabidhi viti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jangwani Christina Luoga ikiwa ni msaada wa Ukumbi wa Starehe kilichopatikana kusaidia hapo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Maendeleo ya Jamii Brothers To Men  Paul Kivumbi akizungumza na waandishi Habari mara baada ya kukabidhi viti na miundombinu ya mabomba kwenda katika vyoo kwenye shule ya msingi Jangwani ikiwa no msaada wa Ukumbi wa Starehe Bar and tiptop Grill iliopo mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Maendeleo ya Jamii Brothers To Men Paul Kivumbi akimkabidhi viti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jangwani Christina Luoga ikiwa ni msaada wa Ukumbi wa Starehe kilichopatikana kusaidia hapo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jangwani Christina Luoga akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka Kikundi cha Maendeleo ya Jamii Brothers To Men.
Ufukiaji wa mabomba kwenda katika vyoo ukifanyika kwenye shule ya msingi Jangwani ukiwa ni msaada wa Brothers To Men.

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv 

KIKUNDI cha Maendeleo ya Jamii kinachoendesha Ukumbi wa Starehe Bar ya Pittop and Grill Mbezi Beach kimetoa msaada wa viti vya walimu pamoja na kutandika mabomba kwenye vyoo vitatu katika Shule ya Msingi Jangwani iliyopo Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Kikundi hicho Paul Kivumbi amesema kuwa hawana budi kuchangia shule hiyo kwani iko Karibu eneo la biashara yao.

Kivumbi amesema kuwa baada ya kufanya utafiti wa kuweza kusaidia walikutana na uongozi wa Mtaa na kukubaliana wasaidie katika Shule hiyo.

Kivumbi amesema kuwa wanaangalia baadae wasaidie bati katika Shule hiyo kwani zinaonyesha uchakavu ambao kama wao hawakubaliani kuona shule hiyo ikiwa katika mazingira yasiyoridhisha.

"Sisi kama jamii tunayoizunguka shule ni wajibu wetu kusaidia kwani ni watoto wetu wanasoma ambao wanahitaji kusoma mazingira yaliyo bora na hakuna kila kitu tuiachie Serikali"amesema Kivumbi.

Aidha amesema kuwa watu wengine waguswe na shule hiyo kwa kusaidia maeneo mbalimbali kwani changamoto katika shule hazikosekani.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jangwani Christina Luoga amesema kuwa kikundi hicho kimefanya jambo zuri kwa kutandika mabomba kwenda vyooni.

Amesema wanafunzi wamekuwa wakichota Maji na kupeleka hiyo ni changamoto kwa wasichana wakati wakiwa katika kipindi cha hedhi.

Amesema kuwa wameona mbali sana Kama uongozi wa shule unashukuru kwa kuonyesha wanajali walimu pamoja na wanafunzi.

Mkuu wa Shule hiyo ametoa wito watu wengine wanaweza kuendelea kusaidia sehemu ambazo zinatakiwa kuboreshwa huku Serikali ikiwa katika mikakati ya uboreshaji wa shule .

No comments: