BARAZA LA WAWAKILISHI KUANZA MEI 5, ZANZIBAR

 


KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem amesema Mkutano wa Tatu wa Baraza la Kumi la Wawakilishi unatarajiwa kuanza Siku ya Jumatano Tarehe 05/ Mei 2021 Saa tatu asubuhi huko Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Amesema Mkutano huo utajadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa 2021/2022 na jumla ya maswali ya msingi 218, yataulizwa  na kujibiwa.

Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje Kidogo na Mji wa Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu kuanza kwa shughuli za Mkutano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Utakaojadiliwa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Aidha  amesema kutakuwa na Miswada miwili  ya Sheria  itawasilishwa na kujadiliwa ambayo ni Mswada wa sheria ya Fedha pamoja na Mswada wa Sheria ya kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022.

Alifahamisha kuwa katika Mkutano huo kutakuwa na majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka wa fedha 2021 hadi 2022.pamoja na  Miswada  ambayo inatarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza katika Baraza hilo.

Hata hivyo amesema kutakuwa na Kiapo cha Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Pandani Profesa Omar Fakih Hamad .

No comments: