RC HAPI AWATAKA MAKANDARASI KUMALIZA KAZI KWA WAKATI
JOSEPH MPANGALA -IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameitaka kampuni SINO HYDRO ya Inayotekeleza ujenzi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa Kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo kwa Viwango na wakati kutokana Pesa zote kukamilishwa kupewa.
Hapi ameyasema hayo alipotembelea Mradi wa ujenzi Huo Unaogharimu Shilingi Billion 41 na unatarajiwa Kukamilika June 23 mwaka 2022.
“Wakandarasi wababaishaji natakanitume salam kwao hawatakuwa na nafasi kwenye Mkoa wetu wa Iringa na hawatakuwa na nafasi kwenye serikali hii habari za kuomba kuongezewa muda kuchelewesha miradi,kufanya miradi chini ya kiwango hayo hayatakuwa na nafasi tutakuwa wakali zaidi tulivyokuwa jana”Ally Hapi wakati akikagua Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa
Awali Ujenzi huo Ulisimama kutokana na Kuchelewa kwa Malipo ya Fidia za Mali za wakazi wa kata ya Nduli ambapo Ujenzi Huo Unafanyika.
No comments: