HALMASHAURI KUWATUMIA WAATALAMU KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI.


Halmashauri nchini zimetakiwa kuwatumia wataalamu wanaohitimu mafunzo ya mipango miji na wapimaji wa ardhi mjini na vijijini ili kuweza kutatua migogoro ya ardhi inayosababishwa na kutopimwa ardhi katika maeneo mbalimbali kwenye Halmashari.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo wakati wa akimwakulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Merry Makondo katika maafali ya 39 ya kutunuku vyeti wahitimu wa fani mbalimbali wapatao 394 wa chuo cha Ardhi Morogoro.

 Mhandisi Kalobelo amesema kama wataalamu wanaozalishwa na vyuo Ardhi chini kama watatumik vizuri na Halmashauri za Mikoa katika upimaji wa ardhi migogoro mingi itapungua kwani kila mtu atakuwa anamiliki ardhi iliyopimwa na kumilikiwa kisheria.

“Ni aibu kwa Mkoa kama Morogoro kuendelea na migogoro ya ardhi wakati chuo cha kuzalisha wataalamu wa kupanga na kupima kipo hapahapa. Naagiza kabla ya mwaka huu kuisha Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro ziwe na mpango mkakati wa kuona jinsi gani ya kushirikiana na chuo cha ardhi Morogoro na kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapangwa,kupimwa na kumilikishwa”.alisema Mhandisi Kalobelo.

Aidha Mhandisi Kalobelo ametumia maafali hiyo kutoa wito kwa wadau,mamlaka na tasisi mbalimbali kutenga fedha kwaajili ya kuweka mazingira wezeshi kwa wataalamu wanaopima Ardhi kwenye Halmashauri zao.

Kwa upande wake kaimu mkuu chuo cha Ardhi Huluma Lugala amesema chuo kimeweza kuongeza udahili kutoka wananfunzi 400 mpaka kufikia wanafunzi 500 ikiwa ni ongezeko la asilimia 23 ya wananfunzi wote walioko chuoni hapo.

Pia amesema mbali na kuzalisha wataalamu wa kupanga na kupima pia chuo cha Ardhi Morogoro kimekuwa kikishiriki katika kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu na kufanya miradi ya urasimishaji ambayo hadi sasa inatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Morogoro.  

Naye Makamu mwenyekiti Bodi ya chuo Zakaria Ibrahim amesema kuwa chuo hicho kimeendaa mpango mkakati wa mfumo wa mafunzo ambao utaweza kuzalisha wataalamu wengi na wenye ujuzi zaidi katika masuala ya upimaji wa Ardhi.

No comments: