wanawake wajasiriamali wajichangisha kununua kitanda cha kujifungulia na kukabidhi zahanati ya Likokoma wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara
Na Mwaanidishi Wetu Mtwara
WANAWAKE wajasiriamali wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wamechanga na kununua kitanda cha kujifungulia wanawake kwa ajili ya kusaidia zahanati ya Likokona ambayo inapokea wanawake 4 mpaka 6 kwa siku huku ikiwa na kitanda kimoja cha kujifungulia,
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kitanda hicho, Mganga Mfawidhi wa Zahana hiyo Rehema Akili amesema zahanati hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1974 inapokea wanawake zaidi ya 300 kwa mwaka huku wanawake wengine wakilazimika kujifungulia sakafuni.
Amesema kwa mwaka 2018 zahanati hiyo ilipokea wanawake 254 na kwa mwaka 2019 walipokea 229 na huku 2020 na wakipokea wanawake 330.
Amesema zahanati hiyo inahudumia vijiji 4 na kwamba ina watumishi 3 wakimo wauguzi wawili pekee. Ameiomba serikali na wadau wengine kusaidia hiyo zahanati katika kuchangia vitanda na vifaa vingine ikiwemo ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama ambayo kwa sasa inajengwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
“Changamoto zetu kubwa ni idadi ndogo ya watumishi ambapo tuna watumishi watatu wakiwemo wauguzi wawili tu, uhaba wa majengo wa kutolea huduma,” alisema Akili.
Aliomba zahanati hiyo kusaidiwa katika kujenga jengo la wazazi kuboresha huduma za akina mama na kuongeza watumishi ili tuweze kutoa huduma bora kwa jamii yetu.
Pia aliomba serikali kuwajengea kituo cha afya kama walivyoahidi kwenye ilani ya CCM kuwa watawajengea kituo cha afya ili kuboresha huduma za afya. Pia aliwashukuru akina mama hao kwa kuguswa kuchangia kitanda ambacho kwa sasa kitasaidia zahanati kupokea wanawake wanaojifungua.
Kwa upande wake, Mratibu wa kikundi cha akina mama wajasiriamali Eloisi Malisa amesema wanawake hao waliamua kuchagishana na kununua hicho kitanda ili kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli katika kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumeamua kuchangishana kama akina mama ili kuunga juhudi za Raisi ambazo anafanya haswa katika kuboresha miundombinu ya afya hususan majengo na sisi tukaona tusaidie katika kuchangia vifaa tiba kama kitanda kusaidia akina mama wa Likokona,” amesema.
No comments: