PERAMIHO INA FURSA YA MAWASILIANO - MHANDISI KUNDO


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea (mwenye suti nyuma) akipata maoni ya wananchi katika kata ya Ipitimbi  katika Jimbo la Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza katika mnara uliyojengwa na Vodacom kwa Zabuni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF.)
Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akitoa mikakati waliojiwekea katika utoaji huduma za mawasiliano wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mhandisi Kundo Andrea.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea  akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mkoani Ruvuma.
Wananchi wa Kata ya Ipitimbi wakiwa katika mkutano wa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea wakati alipofanya ziara ya  kujua changamoto ya mawasiliano katika katika kata hiyo.
Mkazi wa kijiji wa Ipitimbi Jimbo la Peramiho Silvanus Njovu akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea   alipofanya ziara katika Jimbo hilo.


*TCRA waelezea maendeleo makubwa ya huduma za Internet Ruvuma.

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv Songea

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa Jimbo la Peramiho lina fursa za kibiashara za mawasiliano na kutaka watoa huduma wa kampuni za simu kujenga minara.

Kundo aliysema wakati alipofanya ziara katika Jimbo hilo na kutembelea sehemu zenye changamoto za Mawasiliano katika kijiji vilivyo  Kata za Mpitimbi pamoja na Ndokosi 

Mhandisi Kundo amesema kuwa kufika katika Jimbo  hilo ni kutaka wananchi wafurahie huduma za mawasiliano ambazo katika kufikia asilimia 80 mwaka 2025.

Kundo amesema jimbo la Peramiho linahitaji minara ya 3G na 4G kwa mahitaji ya mawasiliano yamekua na kuhitaji matumizi ya data.

Amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameanzisha Wizara ikiwa ni kutaka kutatua matatizo ya mawasiliano.

Kundo amesema kuna miradi mingi ya mawasiliano inayoendelea ni pamoja na mfumo postal code ambapo huduma ya vifurushi zitakuwa kiganjani.

Nae Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John ameeleza namna huduma za mawasiliano ya internet zilivyozidi kuenea mkoani Ruvuma ambapo Wilaya ya Songea peke yake ina jumla ya minara 71 ya mawasiliano ya simu, ikiwepo ya 4G inayopatikana katika baadhi ya maeneo ikiwepo Peramiho, Mpitimbi na Litapwasi. 

Mhandisi John amesema huduma ya 4G katika kijiji cha Litapwasi ni ishara kuwa wananchi wa vijijini wanaendelea kuunganishwa kwenye mawasiliano ya data kuelekea kutimizwa lengo la zaidi wa watumiaji wa Internet asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

No comments: