NAIBU WAZIRI KUNDO: POSTA MASTA MKUU AJITATHIMINI KATIKA NAFASI HIYO
*Zaidi ya sh.bilioni 3 zilizotakiwa kwenda katika makato ya hifadhi ya jamii zaishia mifukoni ya watu
Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog - Songea
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amemtaka Posta Masta Mkuu ajitathimini kwa nafasi yake.
Kundo ameyasema katika ziara za kutembelea mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa wafanyakazi kukunyanyaswa na shirika la Posta na kufanya Shirika hilo kudumaa.
Amesema katika unyanyasaji huo ni pamoja na kukosesha mambo ya msingi kwa makato mbalimbali yanayotakiwa Shirika limekuwa halipeleki.
Mhandisi Kundo amesema kuwa kuna zaidi ya sh.bilioni tatu hazijapelekwa katika mifuko ya hifadhi ya Jamii lakini wafanyakazi wakiwa wamekatwa.
Amesema kutokana na shirika hilo kushindwa kupeleka makato kunashusha wafanyakazi kujituma kwani wakienda kuchungulia makato yao hawaoni kitu chochote.
Aidha amesema kuwa wafanyakazi wanaokuwa na uwezo wa kuhoji na kutaka Shirika hilo lifike mbele wamekuwa wakihamishwa kwenda pembezoni ili wachache waendelee na michezo yao.
"Hatuwezi kuwa na shirika lisilojali rasilamali watu wa huku hukuna mabadiliko yanayoonekana sasa mwisho wao umefika katika Wizara ya Mawasiliano" amesema Mhandisi Kundo.
Hata hivyo amesema kuwa wafanyakazi mizigo ndio wanawafanya madudu makubwa ambayo Shirika kila ukiangalia halioneshi mwanga wa kuweza kutengeneza faida ya kuweza kwenda katika huduma za jamii.
Naibu Waziri amesema kuwa matatizo yanayoonekana katika Shirika la Posta ni ugonjwa wa kudumu ambao hakuna mtu wa kuweza kubadilisha Shirika hilo.
Amesema ofisi za Mikoa haziendani kabisa kwa ajili ya kufanya ushindani wa kibiashara kutokana na udumavu wa mawazo na wenye uwezo katika Shirika kuonekana wanaharibu mipango ya watu.
No comments: