MKUU WA MKOA WA SHINYANGA APONGEZA RUWASA KUMTUA MAMA NDOO YA MAJI KICHWANI.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akikagua mradi wa maji uliopo mji mdogo Segese ulioko katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama kulia kwake ni Meneja wa TARURA Shinyanga Eng. Julieth Payovela na kushoto kwa ni Meneja wa TARURA Kahama Bw.Maduhu Magili.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akikagua mradi wa maji wa Kakola- Bushingwe ulioko katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama uku wananchi wa Kata ya Bulyanguru wakishhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akishuhudia mwananchi mmoja wa kata ya Bulyanguru ambaye alikuwa akichota maji kufuatia kukamilika kwa mradi wa maji wa Kakola- Bushingwe ulioko katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama.
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu- Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack jana alifanya ukaguzi wa miradi mitatu ya maji iliyoko Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama yenye thamani ya takribani Bil.4.7 ambayo imekamilika na tayari kwa kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Halmashauri hiyo wapatao elfu 30.
Akiongea na Wakazi wa Kata ya Bulyanguru iliyoko Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama alipofika kujionea kukamilika kwa Mradi wa Maji wa Kakola- Bushingwe Bi. Telack aliwataka wakazi hao kuanza kujiunganishia maji majumbani mwao kwakuwa maji hayo ni ya uhakika.
Bi. Zainab Telack amewataka wakazi hao kutokuwa na wasiwasikuhusu kutosheleza kwa maji hayo na kuwahakikishia kuwa kuna mradi mwingine wa maji kutoka Ziwa Victoria ambao utapitia maeneo hayo na ivyo kuongeza nguvu ya upatikanaji maji zaidi katika kata hiyo.
Naye Meneja wa RUWASA Mkoani Shinyanga Eng. Julieth Payovela amesema miradi yote mitatu ya maji inayoendelea katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga itakamilika kwa 100% ifikapo Julai mwaka huu na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi takribani elfu 30.
Bi. Payovela alisema kuwa utekelezaji wa Miradi ya RUWASA inakumbana na changamoto ya wazabuni kushindwa kuwasilisha vifaa vya kuunganisha maji kwa wakati na hivyo kuchelewasha baadhi ya miradi kukamilika kwa wakati na kuongeza kuwa kadiri muda unavyokwenda suruhisho la changamoto hiyo litakwisha.
Aidha Mkazi wa Kata ya Bulyanguru Bi. Pili Zuberi ambaye tayari ameanza kunufaika na huduma ya maji hayo hakuficha furaha yake na kusema kuwa mara baada ya kuweka maji nyumbani kwake aliweza kuoga mara tatu na kuongeza kuwa kabura ya kuwepo kwa mradi huo alikuwa akisafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
Naye Diwani wa Kata ya Bulyanguru Bw. Shija Joseph alisema kuwa hatua iliyofikiwa ya hutoaji huduma ya maji ni kubwa na kuna mwitikio mkubwa wa watu kujiunganishia maji majubani kwao na ni matarajio yake kuwa maji hayo pia yataweza kufika kwa vijiji jirani na kata hiyo.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa kutembelea miradi ya maji inayoendelea chini ya RUWASA inakuja katika Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani na upatikani wa maji katika kwa wananchi waishio vijijini ni hatua muhimu kwa wanawake nchini kwani upatikanaji wa maji hayo unachangia kwa kiasi kikubwa ya adha ambayo wamekuwa wakiipata ya kufuata maji umbali mrefu.
No comments: