Mchungaji Dankton Rweikila atoa sadaka yenye thamani ya Mil. 10 kwa wajane, wazee , watoto yatima na wasiojiweza Chanika
Na Linda Shebby
MCHUNGAJI Dankton Rudovick Rweikila wa Kanisa la 'Power of God Fire Church" ililoko Chanika Jijini Ilala ametoa sadaka kwa wakaazi 700 wa eneo hilo na viunga vyake ambao hawana uwezo ambao ni watoto yatima , wajane, wazee, walemavu huku ikielezwa kuwa msaada huo una thamani ya Shilingi Mil. 10.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kutoa msaada huo , alisema kuwa amewiwa kutoa kwa watu wasiojiweza huku ikiwa na lengo la kujenga upendo huku wakienda sambamba na mwaka wa kupangusa machozi kwa makundi mbalimbali ya watu ambao hawana uhakika wataishi vipi na waliopoteza mataumaini kwani miongoni mwao wapo ambao hawana uhakika kuwa watakula nini.
" Huu ni mwaka wa kupangusa machozi hivyo tumekula nao chakula pamoja na tutakuwa tunafanya hivi kila mwaka kwa kutoa sadaka hii samvamva na kuwapa zawadi za vyakula ikiwa ni unga na mchele ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wetu wa awamu ya tano Dokta John Pombe Magufuli kama mjuavyo kwamba yeye anawajali na kuwapenda sana watu ambao ni wa hali ya chini amekua akiwapa faraja na kuwathamini katika kila hali na wote tunaona jinsi anavyoguswa na kuundi hili katika jamii yetu"alisema Mchungaji huyo.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa Wachungaji wa Makanisa mengine nchini kuwa wamuunge mkono Rais Magufuli kwa kuwajali wanyonge kote nchini na wakati huohuo amewata watekeleze wito wao walioitiwa na wasiliiachie jukumu hili la kuwajali watu wasiona uwezo kwa serikali .
No comments: