MBUNGE AJA NA MKAKATI MZITO KUKOMBOA WANAWAKE DAR

 

 

*******************************************

NA MWANDISHI WETU

MBUNGE wa  Viti Maalumu Janeth Mahawanga, amesema  anatarajia kuja na  Mkakati wa Dira ya Maendeleo   ya Kiuchumi kwa wanawake atakaouwasilishwa  katika Kongamano  la Siku ya Wanawake Duniani lililopangwa  kufanyika Machi 13 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudentia Kabaka anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kongamano hilo limeandaliwa na Mbunge  huyo  kupitia UWT , Mkoa wa Dar es Salaam na litafanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Akizungumza, Jijini Dar es Salaam, Mbunge Janeth, alisema, wataitumia siku hiyo kupanga na kuwasirisha Dira ya Maendeleo ya Kiuchumi kwa Wanawake katika Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Kusudi   ni  kumfanya mwanamke  ajiamini zaidi na kumkomboa kiuchumi, yeye, jamii yake na taifa kwa ujumla,”alisema Janeth.

Mbunge huyo alisema hafla hiyo itahusisha  wanawake kutoka makundi mbalimbali, kama vile makundi ya watu wenye ulemavu, mabinti wa vyuo vikuu na kidato cha sita.

“Kwani ni muhimu   kuwashirikisha  pia mabiti ambao ni viongozi wa  kesho ili  kuwajengea uwezo sasa hivi na kuwafanya nao wajiandae  kuwa wajasiriamali na wawekezaji ndani ya taifa lao, sambamba na kuwashirikisha  katika masuala ya msingi yanayo mgusa mwanamke,”alibainisha.

 

Janeth alibainisha, siku hiyo  kutakuwa na midahalo mbalimbali ambayo itahusu  wadau na watalam  wabobezi  katika masuala yote yanayogusa  shughuli za  kumkomboa  mwanamke kiuchumi hasa kwa kuzingatia  serikali inapambana kuhakikisha wanawake na vijana wanamiliki viwanda  ambavyo vitakuwa mkombozi  kwenye  jamii  yetu,”salibainisha Mbunge huyo.

Alitaja mambo ya msingi yatakayo jadiliwa ni  kukutana na wadau, tasisi na mashirika yanayojiuhisha na masuala ya  kuwezesha wanawake kiuchumi.

“Kuzitambua shughuli  za taasisi hizo na  jinsi ya kupata fursa kutoka kwa wadau hao. Kupeana maarifa  ya kumkomboa  mwanamke kifikra, kijamii na kiuchumi kupitia  UWT na  jinsi ya  kumshirikisha mwanamke  katika uchumi wa viwanda vidogo, ujasirimali na afya,”alifafanua.

Mambo mengine ni  masuala yote yanayo husu elimu ya ujasiriamalim usafi wa mazingira na kuzitambua haki  za msingi za kisheria  ambazo mwanamke huwa anakosa  kwa kuto kuzijua  hasa katika kumiliki ardhi, mirathi, mali  na malezi ya watoto

“Pia namna ya kuzitambua fursa  zinazotuzunguka  ndani  na nje ya mkoa wa Dar es Salaam,  ambazo zitatuongezea  vipato na kuimarisha uchumi wetu. Aidha kupata fursa ya kuwakutanisha wanawake waliofanikiwa,”alifafanua  Janeth.

Kauli mbiu ya Siku bya Wanawake Duniani ambayo Kilele chake ni leo ni Wanawake  katika uongozi: Chachu kufikia Dunia yenye usawa.

Siku ya  Wanawake Duniani chimbuko lake ni mwaka 1911 kufuatia  maandamano ya  wanawake wafanyakazi wa sekta za viwanda  nchini Marekani  waliokuwa wakipinga mazingira duni  ya kazi, unyanyasaji wa kijinsia na maslahi madogo.

No comments: