HALMASHAURI MKOANI TABORA ZATAKIWA KUPIMA NA KUTENGA MAENEO YA UWEKEZAJI
………………………………………………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI Mkoani Tabora zimeagizwa kupima na kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuhamasisha na kuvutia wawekezaji toka ndani na nje ya Nchi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokuwa kikipitia mapendekezo ya bajeti ya 2021/22.
Alisema maeneo hayo yatolewa kwa Wawekezaji bila malipo na visiwepo vipingamizi yasiyokuwa na msingi wakati wa utoaji maeneo kwao ili Mkoa wa Tabora upate viwanda vingi.
“Tunataka tuwatengenezee Wawekezaji mazingira mazuri waje kwa vingi,tunaka tuwe na viwanda vikubwa ambavyovitasaidia kuinua Mkoa wetu na kutoa ajira kwa vijana wetu…katika hili lazima tuwe na mtazamo wa pamoja kama Mkoa wa kuvutia wawekezaji wengi” alisisitiza
Alisema sanjari na upimaji na utengaji wa maeneo hayo ni vema kukawepo mashamba makubwa ya pamoja ya mazao(block farm) ya mikorosho, miembe , alizeti na maeneo ya ufugaji nyuki ili kupata malighafi za kutoshwa kwa ajili ya viwanda.
Aidha Dkt. Sengati alikipongeza Kijiji cha Karangasi wilayani Uyui ambacho kimeanza kutenga maeneo makubwa kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha korosho.
Akichangia wazo hilo Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi Brigedia Jenerali Julius Gambosi alisema katika zoezi upimaji maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni vema Halmashauri zikakumbuka kutenga maeneo kwa ajili ya Jeshi ili liwe na eneo masuala ya ulinzi ikiwemo miradi mikubwa inayotekelezwa.
Alisema ni vema kwa kila inapokuwepo miradi mingi ya maendeleo kukatengwa maeneo kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi na uendelevu wake.
Katibu Tawala Msaidizi Rukia Manduta alisema kati ya fedha hizo mishahara ni bilioni 179.2, matumizi mengineyo(oc) bilioni 25.3, miradi ya maendeleo ni bilioni 87.6.
Alisema kwenye miradi ya maendeleo bilioni 46.5 ni fedha za ndani na bilioni 41 ni fedha kutoka nje.
No comments: