BILIONI 123.3 KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI 649 MKOANI TABORA IFIKAPO 2025

 

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Tabora Hatari Kapufi (aliesimam)alitoa taarifa jana ya utekezaji wa miradi ya uboreshaji wa huduma ya maji safi na salama vijijini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Baadhi ya wadau wakijadiliana jana kuhusu utekezaji wa miradi ya uboreshaji wa huduma ya maji safi na salama vijijini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo .

Picha na Tiganya Vincent

………………………………………………………………………………………..

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) inatarajia kutumia shilingi bilioni 123.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye vijiji 649 vya Mkoa wa Tabora.

Miradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ambapo Wilaya zitakazonufaika ni Uyui, Sikonge, Kaliua, Igunga, Nzega na Urambo.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tabora Hatari Kapufi alitoa taarifa hiyo jana wakati wa kikao cha wadau cha kujadiliana mikakati ya uboreshaji wa huduma za upatikanaji wa maji vijijini.

Alisema utekelezaji huo unazingatia maagizo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa mwaka 2020 hadi 2025 na watarajia kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama vijijini kutoka wastani asilimia 62.4 kwa sasa na kufikia 85 ifikapo 2025.

Kapufi alisema kwa Wilaya ya Uyui wanatarajia katika cha miaka mitano ijayo wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 16.7 ambazo zitawezesha kutoka vijiji 55 hadi kufikia 188 ambavyo vitakuwa na uhakika wa maji safi na salama ifikapo 2025.

Alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya watu wanaopata maji safi na salama kutoka 184, 061 na kufikia 415,621 katika kipindi hicho.

Kapufi alisema kwa upande Wilaya ya Sikonge wanatarajia kutumia kiasi bilioni 18.2 ambapo fedha zitaongeza vijiji vinavyopata maji safi na salama kutoka vitano hadi kufikia 45.

Alisema wilayani Nzega wanatarajia kufikisha huduma ya maji safi na salama katika Vijiji 100 kutoka 22 kwa gharama ya shilingi bilioni 48 na kunufaisha wakazi  298, 309.

Kapufi alisema wilayani Kaliua wanatarajia kuvifikia vijiji 155 kutoka 78 kwa gharama ya bilioni 10.1 ambapo wakazi 495,325 ndani ya kipindi hicho.

Meneja huyo wa Nkoa alisema kuwa wanatarajia kutumia shilingi bilioni 17.2 wilayani Igunga kwa ajili ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 226,859 kwenye vijiji 59

Aliongeza kwa upande wa Wilaya ya Sikonge wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 12 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi 113,675 katika vijiji 102.

No comments: