BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA MABATI 105 KUKARABATI WODI YA WATOTO HOSPITALI YA RUFAA LIGULA MKOANI MTWARA

 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

BANK ya NMB Kanda ya Kusini imetoa mabati 105 yenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000/-) kwa hospital ya Rufaa ya Ligula Mkoani Mtwra kwa ajili ya kusaidia uongozi wa hospital hiyo kukarabati wodi ya watoto ambayo kwa sasa inafanyiwa matengenezo ili kuiboresha zaidi.

Msaada huo umetolewa jana na uongozi wa Bank hiyo ukiongozwa na Meneja wa Kanda Bi Janeth Chango ambaye alisema msaada huo wa mabati ni sehemu ya jukumu la NMB katika kusaidia upatikanaji wa huduma bora za afya kwa jamii.

Amesema moja ya jukumu la NMB ni kusaidia katika sekta ya afya kwa kutoa vifaa mbalimbali vikiwemo vya matibabu, vitanda vya kujifungulia kwa akina mama, vifaa vya ujenzi za wodi.

Katika sekta nyingine kama vile elimu Bank hiyo pia imekuwa ikitoa msaada wa viti na madawati kwa ajili ya wanafunzi. Mwishoni mwa mwaka jana bank hiyo pia ilitoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo chakula kwa waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha siku mbili mfululizo mkoani mtwara.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Dunstan Kyobya, Katibu Tawala wa Wilaya Thomas Salala aliipongeza Bank hiyo kwa kuwa mstali wa mbele katika kusaidia serikali na jamii kwa ujumla kuboresha huduma za jamii mkoani hapa.

“Kwa niaba ya Mkuu wetu wa Wilaya, napenda kuipongeza bank ya NMB , wamekuwa wadau wakubwa Sanaa katika kusaidia serikali kuboresha huduma mbalimbali za kijamii, napenda kualika na wadau wengine waige mfano huu wa NMB,” amesema.

Akizungumzia suala la afya katika hospital hiyo, Salala amehakikishia NMB kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha wodi hiyo ya watoto. Amesema serikali imedhamiria katika kuboresha huduma za afya kwa kuongeza watumishi na kuhakikisha miundombinu bora hivyo msaada huo wa NMB utakuwa chachu katika kusaidia juhudi za serikali.

Kwa upande wake Daktari wa hospital hiyo Daktari Rebikieki Kisambh amesema hospital inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu yasiyokidhi mahitaji kwa wagonjwa na watumisho na kuathiri utoaji wa huduma bora za afya. Alisema majongo mengi yamekuwa ni chakavu na yanahitaji maboresho.

Amesema mbaoresho ya majongo hayo na miundombinu yanahitaji jumla ya shilingi billioni 3.6. Alisema moja ya Jengo  linalohitaji ukarabati ni wodi ya watoto ambapo ukarabati wake unahitaji shilingi milioni , 24.8. Ukarabati wa wodi huo ulianza mwaka jana Machin a mpaka sasa marekebisho yamekamilika kwa asilimia 50.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara Thomas Salala (Katikati) akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Dunstan Kyobya Kwa ajili ya kupokea mabati 105 yaliyotolewa na banki ya NMB Kwa hospital ya Rufaa ya Ligula Mkoani Mtwara Kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya watoto katika hospitali hiyo. Kushoto ni Meneja wa Bank hiyo Kanda ya Kusin Bi Janeth Chango na kulia ni Daktari Robikieki Kisambu wa hospitali hiyo.

No comments: