WATU 17 MIKONONI MWA POLISI

JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limewatia mbaroni watu 17 kwa tuhuma za makosa mbalimbali, wakiwemo watuhumiwa sugu wa mauaji ya familia, makosa ya ukatili wa kijinsia pamoja na ubakaji katika msako mkali wa kata kwa kata wa kuzuia vitendo vya uhalifu.

Sambamba na hilo jeshi la polisi limewatia mbaroni watuhumiwa hao na limekamata vitu vilivyoporwa zikiwemo gari, Luninga, Simu za mkononi, Pikipiki, Dawa za kulevya pamoja na mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya moshi aina ya gongo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro, amemtaja mmoja kati ya watuhumiwa sugu wa mauaji kuwa ni Bakari Hamis mkazi wa mlimani “B”, anayetajwa kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji.

Aidha amewataja watuhumiwa sugu wa makosa ya ubakaji ni Said Yusuph mwanafunzi, Said Ramadhani mkazi wa Buswelu, Paschal Boniface mkazi wa Mwakarundi, Hamis Hussein mkazi wa Kirumba pamoja na Shaban Sarehe mkazi wa bezi kisiwani Ukerewe.

No comments: