WACHEZAJI, KIONGOZI WETU WANAPEWA VIDONGE VINAWAUMIZA KICHWA - NAMUNGO FC
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Mwenyekiti wa Timu ya Namungo FC, Hassan Zidadu amesema Wachezaji watatu na Kiongozi mmoja wa timu hiyo ambao wamebaki nchini Angola bado hawajapimwa tena Virusi vya COVID-19 hadi sasa, amesema wanaamini kuwa ni siasa za mpira na sio maambukizi ya Corona.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Zidadu amesema Wachezaji hao na Kiongozi huyo wanadia wanapewa vidonge ambavyo vinawasabishia maumivu ya kichwa, amesema wanafanya utaratibu wa kuhakikisha wanaletwa mjini ili kuwa na ukaribu na kupata huduma kwa urahisi.
“Wapo KM 260 kutoka mjini lakini kwa sasa tunafanya utaratibu wapate Hoteli ili wasogee wapate huduma kwa ukaribu, kwa sasa wapo mbali sana na Balozi wetu wa Heshima nchini Angola”, ameeleza Zidadu
“Mtendaji Mkuu wa timu, Omar Kaya wanampa Vidonge anapata maumivu ya Kichwa, mbaya zaidi inampelekea kupata Shinikizo la Damu (BP), kwa sasa pia wanasubiri BP ishuke warudi mjini”, amesema Zidadu
Zidadu amesema Wachezaji waliobaki nchini Angola wanaendelea na mazoezi kama kawaida ili kuendelea kujiweka sawa na mazingira ya kimichezo, amesema Kikosi cha Namungo kinafikiria kufanya vizuri zaidi katika michezo hiyo itakayochezwa nchini Tanzania.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeamua mchezo wa Namungo FC ya Tanzania dhidi ya CD DE Agosto ya Angola utachezwa nchini Tanzania kati ya Februari 21 na 26, 2021. Mchezo wa kwanza Agosto watachagua Uwanja kati ya Azam Complex, Chamazi au CCM Kirumba, Mwanza wakati mchezo wa pili Namungo FC watachagua Uwanja ambapo utapigwa Azam Complex, Chamazi.
Mwenyetiki wa timu ya Namungo FC, Hassan Zidadu akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Wachezaji wao watatu na Kiongozi mmoja waliobaki nchini Angola wakidaiwa kuwa na maambukizi ya COVID-19.
No comments: