MBUNGE WA MKURANGA AENDELEA NA JUHUDI ZA UTEKELEZAJI AHADI JIMBONI
NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega, amekabidhi bati 90 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nane ya shule ya sekondari Mkwalia Kitumbo, mifuko ya saruji 75 ya ujenzi wa shule ya sekondari Kipalang'anda, mifuko 50 ya saruji shule ya msingi Kinene na jezi za mpira wa miguu kwa timu 6 na mipira 6 kwa vijana.Amekabidhi vifaa hivyo wakati alipofanya ziara ya siku moja jimboni kwake Mkuranga.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega akishiriki kuchimba msingi ujezi wa shule ya Sekondari Magoza kata ya Kaparang'anda ambapo amekabidhi mifuko ya saruji 75 na kiasi cha fedha zaidi ya laki Saba.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega (watatu kulia) akikabidhi mifuko 75 ya saruji kwa viongozi wa kata ya Kaparang'anda kwaajili ya kujengea shule ya kata hiyoo.
Madiwani wakishiriki kuchimba msingi kuunga mkono juhudi za maendeleo katika shule ya msingi Magoza kata ya Kaparang'anda.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo na Mwenyekiti wa Halmashauri Mkuranga, Mohamed Mwela wakishiriki kuchimba msingi wa shule ya msingi Magoza kata ya Kaparang'anda.
Muonekano wa majengo ya Sekondari ya kata ya Mkuranga.
Wananchi wa kata Kaparang'anda wakiendelea na kazi.
No comments: