MBUNGE SANGA, IDARA YA MAJI WILAYA NA KAMATI YA MAJI IPELELE WAANZA MIKAKATI YA KUTAFUTA CHANZO KINGINE CHA MAJI KUONGEZA WINGI WA UPATIKANAJI WA MAJI

Akiwa ameongozana na Kamati ya Maji (Jumuia ya wanufaika maji) Ipelele na wataalamu wa Maji kutoka Idara ya Maji Wilaya ya Makete. Mbunge wa Makete Ndg Festo Sanga ameshirikiana nao kutafuta uwezekano wa kuongeza chanzo kingine cha maji ili kuongeza wingi wa Maji kwenye Kata ya Ipelele ambayo kwa muda sasa imekuwa na maji ya kusuasua.

Wakiwa kwenye safu za uwanda wa Mbuga ya Kitulo, Sanga ametoa maagizo kwa Idara ya maji wilaya, kupima usalama wa Maji wanayotumia wanaanchi wa ipelele madai ya Wananchi kuwa maji hayo yanachanganyana na maji yanayotoka barabarani.,Pili kuanzisha kwa mpango mkakati wa kuongeza chanzo kingine cha Maji ili kuondoa kero ya maji kwa Wananchi hao, tatu kukifanyia ukarabati chanzo cha zamani cha maji ikiwepo kuweka fensi na nyavu za kuzuia wadudu waisiingie kwenye bomba la maji.

Idara ya maji Makete imeyapokea mapendekezo hayo, na la ukarabati linatarajiwa kukamilika katikati ya mwezi wa pili 2021.

Naye mzee maarufu wa kijiji cha Makeve Mzee Mbwillo asema, "watumishi wa serikali waige kasi ya Rais Magufuli katika utendaji wao, wasisubiri kelele za waanchi ndipo waje kutatua kero,ofisi ya mtumishi wa serikali ni kwenye utatuzi wa kero, hili la maji limegeuka kero na tunaomba maji tupatiwe chanzo kingine ambacho tayari sisi kama kijiji na kata ya ipelele tumeshakibaini huku huku milimani"







 


No comments: