Hospitali ya Temeke kuwa na vyumba sita vya upasuaji

ILI kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wa upasuaji, hospitali ya Temeke iko kwenye mkakati wa kujenga vyumba sita vya upasuaji (theater).

Nuswe Ambokile ambaye ni ...... wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke amebainisha hayo jana wakati akipokea misaada ya dawa na mahitaji mengine ya kibinadamu vilivyotolewa na kampuni ya Meridian Bet.

Msaada huo wa Meridian Bet ulitolewa maalumu kwa baadhi ya wagonjwa wenye uhitaji waliolazwa kwenye hospitali hiyo, kama sehemu ya kampuni hiyo kurudisha kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Nuswe alisema umekuwa na faraja kwao na wagonjwa wenye uhitaji katika hospitali hiyo.

Alisema kuna dawa kama za sindano za vitamin K zinauzwa bei kubwa na kuna baadhi ya wagonjwa hawana uwezo wa kununua.

"Msaada huu kwa kiasi fulani utapunguza changamoto kwa wagonjwa, ingawa sasa hospitali iko katika ujenzi wa theater ili ziwe sita na vyumba vya uangalizi maalumu (ICU) ziwe mbili, ili tuweze kuhudumia wagionjwa wengi wanaofikia hospitalini hapa kwa muda mfupi.

Alisema hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kutoka wilayani Temeke na maeneo jirani ikiwamo baadhi ya mkoa wa Pwani.

Akikabidhi msaada huo Afisa Huduma wa jamii wa Meridian Bet, Amani Maeda alisema ni muendelezo wa kampuni yao katika kurudisha kwa jamii.

"Uwa tunafanya hivi mara kwa mara, leo (jana), tumekuja kwa wenzetu wa Temeke Hospitali na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa, glovu, pempars za watu wazima, gozi, mipira ya kulalia na mahitaji mengine ya kibinadamu," alisema.

Alisema Meridian Bet imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa wahitaji, ambapo imewahi kufanya hivyo kwa wagonjwa wa kansa wa hospitali ya Ocean Road, chama cha Albino Kigamboni, hospitali ya Wazee Kinyerezi na taasisi mbalimbali zenye uhitaji.

No comments: