Zaidi ya wateja milioni 7 wapokea bonasi ya 'Jaza Tukujaze Tena' nchi nzima

 

NIMESHINDA NA MIMI: @iamlavalava akimkabishi mshindi wa Kitochi 4G Smart kutoka Tigo baada ya kuibuka mshindi wa siku kampeni ya #JazaTukujazeTena.
#TumewashaNaTigo

Mhe. Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.awahakikishia wana-mbeya usalama pindi wakiwepo kwenye #WasafiTumewashaNaTigo kama ambavyo tunapowahakikishia Bonus za Dakika, MB pamoja na Bonus kila ukijaza kifurushi chochote #JazaTukujazeTena.
i #JazaTukujazeTena yani kila ukinunua kifurushi Tigo inakujaza Bonus za Dakik, MB na SMS zaidi. Yaan kila mtu ni mshindi. #TumewashaNaTigo



Na Mwandishi Wetu, Mbeya

ZAIDI ya wateja milioni 7, wamefanikiwa kupokea bonasi ya kampeni ya 'Jaza Tukujaze Tena' nchi nzima.

Akizungumza jijini hapa katika hafla ya makabidhiano ya simu kwa washindi wa kampeni ya Jaza Tukujaze Tena, 

Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Aidan Komba, alisema hadi sasa ni zaidi ya wateja milioni 7 wamefanikiwa kupokea zawadi hizo.

Alisema wiki hii, walikua jijini Mbeya kwaajili ya kuwakabidhi washindi simu zao walizo bahatika kushinda kupitia droo iliyofanyika wiki hii ya kampeni ya inayoendelea, inayojulikana kama Jaza Tukujaze Tena.

Alisema kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa nchi nzima mwezi uliopita, imepokelewa vizuri.

"Leo tunayo furaha kukabidhi wateja wetu zawadi zao walizoshinda kwenye droo iliyofanyika wiki hii.

"Tangu tuzindue kampeni yetu mwezi uliopita kwakweli imepokelewa vizuri nchi nzima.

"Kwani hadi sasa wateja wa Tigo nchi nzima wamejazwa bonasi za dakika milioni 460, MB billion 1.9, SMS million 217.

Simu janja zilizotolewa hadi sasa ni 547.

Kwa ujumla hadi sasa wateja zaidi ya million 7 wamekwisha pokea bonasi za dakika,MB na SMS nchi nzima, alisema.

Aliongeza: "Hapa Mbeya napo hamjaachwa sana nyuma katika kujazwa ma-bonasi ya Jaza Tukujaze Tena, 

Kwa ujumla mpaka sasa, Mbeya imeshajazwa 

dakika: 10,820,555, MBs: 40,939,68 na SMS: 7,930,950,".

Alisisitiza kwamba wateja wao waendelea kufurahia bonus za papo hapo za dakika, SMS, pamoja na MBs/GBs za kumwaga kila wanaponunua kifurushi cha siku, wiki au mwezi. 

Alisema na kama haitoshi mteja ataingia kwenye droo ya kushinda Samsung Note 20 na Simu Janja kibao ikiwemo Tecno Kitochi 4G Smart na Itel T20, anachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi chochote cha siku, wiki au mwezi kwa Kupiga*147*00# pia kwa waazaji wa Tigo Rusha na kupita Tigo Pesa, 

"Kila unapojaza Tunakujaza Tena! Vigezo na Masharti Kuzingatiwa," alisema.

No comments: