Wenye Ualbino watamani kujiajiri
UMOJA wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wanaoishi Kigamboni Dar es Salaam wameeleza matamanio yao ya kujiajiri lakini wanakwamishwa na ukosefu wa mtaji.
Mwenyekiti wa umoja huo, Kassim Kibwe amebainisha hayo jana wakati wakipokea misaada ya mahitaji mbalimbali ya kibinadamu kutoka kampuni ya kubashiri ya Meridian Bet.
Msaada huo wa vyakula mbalimbali, kofia na miwani ulikabidhiwa na watendaji wa Meridian Bet wakiongozwa na Mkurugenzi, Chetan Chudasama, oparesheni meneja wa Tanzania, Corrie Borman na meneja ustawi, Aman Maeda.
"Tumefarijika kupata msaada huu na wenzetu wa Meridian Bet kutukumbuka na kutushika mkono wa faraja," alisema Kibwe.
Alisema alibino wengi hawana kazi na hiyo inasababishwa na kutoaminiwa, lakini wana uwezo na vipaji vya kufanya kazi mbalimbali.
"Kwenye umoja wetu tuna watu wa welding, mafundi cherehani na wengine wenye vipaji mbalimbali vya kuchonga na sanaa, lakini hawawezi kujiajiri kwa kuwa hatuna mitaji na kuajiriwa wengi wetu wanaona hatuwezi," alisema.
Alisema kama wangepata ajira za kuwaingizi kipato ingekuwa nafuu kwao kujitegemea na hata kununua mafuta ya ngozi zao ambayo yanauzwa kuanzia Sh 45,000 hadi 120,000.
Meneja ustawi wa Meridian Bet, Aman Maeda alisema wameipokea changamoto yao na watajitahidi kadri wawezavyo kuwasaidia hata kama ni kwa asilimia 50.
"Merdian Bet tuna utaratibu wa kurudisha kwa jamii ndiyo sababu tuko hapa kuwasaidia, changamoto yetu tumeipokea na tutaifanyia kazi," alisema.
Diwani mteule wa Mji Mwema, Kigamboni, Omary Ngurangwa alisema msaada wa Merdian Bet kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wa eneo hilo ni jambo la faraja.
Naye Emmi Ghahae mkurugenzi wa kituo cha Mamas and Papas kinachoshirikiana na watu wenye ualibino Kigamboni alisema sapoti ya Meridian Bet imewapa faraja.
No comments: