WAZIRI WA KILIMO-ZANZIBAR MHE. DKT. SOUD HASSAN AFUNGUA KONGAMANO LA WENYE-VIWANDA NA TAASISI ZA UTHIBITI

 

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo wa Zanzibar Mhe. Soud Hassan akifungua kongamano la biashara kati ya Taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini leo, 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam ambalo limelenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini, Leo 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam ambalo limelenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020.Baadhi ya wadauwa sekta ya Viwanda nchini na washiriki wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini, leo 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam ambalo limelenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020..Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo wa Zanzibar Mhe. Soud Hassan (aliyekaa wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. ,Riziki Shemdoe (aliyekaa wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya TanTrade, Ndg. Edwin Rutageruka wakiwa katika picha na wadau wa sekta ya viwanda nchini na wamiliki wa viwanda nchini waliohudhulia katika kongamano la biashara kati ya Taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini, Leo 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020.

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo wa Zanzibar Mhe. Soud Hassan (aliyekaa wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. ,Riziki Shemdoe (aliyekaa wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya TanTrade, Ndg. Edwin Rutageruka wakiwa katika picha na wakurugezi wa Taasisi za Serikali waliohudhulia katika kongamano la biashara kati ya Taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini, Leo 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020. (Picha na Eliud Rwechungura)

***************************************

Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara hatua inayoongeza kasi ya uwekezaji hasa katika viwanda na biashara, na tayari tumeanza mafanikio yameanza kuonekana.

Ameyasema hayo leo Waziri Wa Kilimo, Umwagiliaji, Mali Asili Na Mifugo – Serikali Ya Mapinduzi – Zanzibar Mhe. Dkt. Soud Nahoda Hassan akifungua Kongamano La Wenye-Viwanda Na Taasisi Za Uthibiti katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho wa Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Serikali imefanikiwa kuandaa na kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara Nchini – BLUEPRINT. Mpango huo umewezesha  maboresho ya tozo, ada na adhabu.  jumla ya tozo, ada na adhabu mia mbili thelathini na mbili (232) zimefutwa au kupunguzwa na Serikali”. Amesema Mhe.Dkt.Hassan.

Aidha Mhe.Dkt.Hassan amesema hatua ambayo imefikiwa miaka mitano kabla ilivyokuwa imetarajiwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Serikali imefanikiwa  kuwavutia wawekezaji makini na mahiri kutoka hapa nchini na nje ya nchi kuja kuwekeza katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Hata hivyo amesema Sekta hiyo imeendelea kuchangia katika Pato la Taifa kwa mfano mwaka 2019 ilichangia kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.45. 

“Kasi ya ukuaji wa thamani ya Uzalishaji Bidhaa Viwandani kwa mwaka 2019 ilikuwa ni Shilingi Trilioni 10.2 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 9.6 mwaka 2018, sawa na kasi ya ukuaji wa asilimia 5.8”. Ameeleza Mhe.Dkt.Hassan.

Nae Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka Ya Maendeleo Ya Biashara Tanzania (Tantrade), Bw. Edwin N. Rutageruka amesema TanTrade imekuwa ikiratibu Kliniki ya Biashara (Business Clinic) kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Uthibiti ili kutatua kero zinazokwaza uzalishaji katika sekta ya viwanda na biashara.

Vilevile amesema Mikutano hiyo inatoa fursa ya kuwakutanisha wanunuzi na wauzaji kujadili na kutathmini kiasi na ubora wa upatikanaji wa bidhaa, malighafi, aina, mashine, teknolojia, kuhifadhi, kusindika na kufungasha kwa kupanga mkakati wa suluhu ya changamoto na kuanzisha mahusiano endelevu ya biashara.

“Mikutano hii imelenga kuhamasisha ustawi wa viwanda hapa nchini kupitia uongezaji thamani mazao yanayozalishwa nchini na bidhaa zake ili kupata masoko endelevu ya ndani, kikanda na kimataifa”. Amesema Bw.Rutageruka.

No comments: